jaridahuru

Mitandao

TEKNOLOJIA: TAMESCO YAWAONDOA WANANCHI WASIWASI KUHUSU MGODI WA KIDATU, YASEMA BADO UNA UWEZO



SHIRIKA la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco), limesema mgodi wa kufua umeme uliojengwa Kidatu Morogoro mwaka 1975, bado una uwezo wa kuzalisha nishati hiyo kwa kiwango cha kutosha.
Kauli hiyo, ilitolewa juzi na Meneja wa Mgodi huo, Injinia Joseph Lyaruu, wakati wa ziara ya wandishi wa habari nchini, kujionea kazi zinavyofanyika katika mgodi huo.

Alisema uwezo huo ulitokana na jitihada za Tanesco kuendelea kuuboresha hatua kwa hatua, ambako hivi sasa katika mgodi huo kumefugwa mashine nne ikilinganishwa na awamu ya kwanza ulipojengwa, ambazo zina uwezo wa kuzalisha umema kwa ufanisi mkubwa ambao unakwenda sambamba na ongezeko la wateja kila mwaka.

“Sio kweli kama mtambo hauwezi kuzalisha umeme kama inavyodhaniwa na baadhi ya watu, bado unao uwezo wa kufanya kazi katika kipindi cha miaka 50, hata nchini India iko mitambo ambayo imefanya kazi zaidi ya miaka 50,” alisema Injinia Lyaruu.

Lyaruu, alisema Watanzania hawana haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu uzalishaji katika mgodi huo, kwa sababu shirika kwa kushirikiana na wahisani wako katika mkakati kubadili baadhi ya vifaa ambavyo vimekuwepo tangu unajengwa.

Akizungumzia kuhusu hali ya maji, Lyaruu alisema Watanzania watarajie kupata huduma hiyo kwa ufanisi na bila kikomo, kwa sababu kipindi hiki maji ya kutosha yapo.

Alizitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni uhaba wa maji, shughuli za kibinadamu karibu na mito inayoingia kwenye mabwawa na uchepushaji wa maji kwa ajili ya kilimo na shughuli nyingine.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu, Rashid Msingwa, alisema mgodi huo una wafanyakazi 104, ambao wanafanya kazi mbalimbali ikiwemo utoaji wa huduma za jamii.

Related

TEKNOLOJIA: TUME YA UCHAGUZI 'NEC' YAENDELEZA UTATA ZABUNI YA MASHINE ZA KUPIGIA KURA 'BVR'

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC), imezidi kuibua utata kuhusiana na gharama halisi za kupata mzabuni wa kuboresha daftari la kudumu la kupigia kura kwa njia ya kielektroniki, (BVR), ba...

TEKNOLOJIA: JE UNAFAHAMU KAMA TAARIFA ZAKO ZA MATUMIZI YA SIMU ZIKO SALAMA? JE MITANDAO YA SIMU INA USIRI?

Ukikutana na Watanzania 10 angalau nusu yao watakuwa na kifaa au vifaa vya mawasiliano kama  simu na kompyuta. Vifaa hivi vimesajiliwa kwa majina yao na taarifa zao nyingine ambazo zinawez...

TEKNOLOJIA: TCRA YAONYA WANAOWADHALILISHA WENZAO KWENYE MTANDAO, YAAHIDI KUWAFIKISHA MAHAKAMANI

MAMLAKA ya mawasiliano nchini ,TCRA, imewaonya wale wote wanaotumia mitando kuchafua na kudhalilisha watu waache mara moja vinginevyo watakabiliwa na mkono wa sheria.   Onyo hilo limet...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item