KIMATAIFA: JARIDA HURU INAWATAKIA WADAU WOTE NDANI NA NJE YA TANZANIA AMANI NA UPENDO
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/09/kimataifa-jarida-huru-inawatakia-wadau.html
Umekuwa kama wimbo sasa, huku, kule utasikia vilio vya kuomba Amani itawale, dunia nzima inalilia Amani. Katika Taifa lenye malengo ya Kujikwamua kiuchumi, ni dhahiri kwamba Amani ndio msingi kwa kuwa ndio njia pekee ya kuweza kuwapa fursa wananchi wake kushirikiana.
Madhara makubwa ya ukosefu wa amani yanaonekana katika kila ncha ya ulimwengu, Darfur, Somalia, Sudan jamani tunaona mifano.
La kuwaomba Watanzania wenzetu, ni kudumisha upendo na mshikamano, kutojali kabila, rangi, uwezo, dini au anapotoka mtu bali kushirikiana kwa kila jambo linaloleta amani na maendeleo katika nchi yetu.
"Iwapo viongozi wa taifa letu watakuwa na Tamaa ya Amani kuliko Tamaa ya Madaraka, Nchi yetu itakuwa na Amani ya Kudumu" Anasema Mkurugenzi wa Jarida Huru.
Hivyo tunapenda kuwatakia kila la kheri katika kuadhimisha siku ya amani Duniani.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania