jaridahuru
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/teknolojia-tcra-yaonya.html
MAMLAKA ya mawasiliano nchini ,TCRA, imewaonya wale wote wanaotumia
mitando kuchafua na kudhalilisha watu waache mara moja vinginevyo
watakabiliwa na mkono wa sheria.
Onyo hilo limetolewa leo(jana) mjini Arusha na kaimu mkurugenzi wa
mamlaka ya mawasiliano nchini TCRC, Dkt, Raynold Mtungahema, alipokuwa
akitoa ufafanuzi wa maswali ya wanahabari kuhusu kuenea kwa picha chafu
zinazowadharirisha watu mbalimbali kwenye mitandao..
Mtungahema, amesema matumizi ya mitandao ambayo sio sahihi ni kosa
la jinai na hivyo wale wote wenye tabia hiyo waache mara moja na
akawataka wanaochafuliwa kupitia mitandao wafungue majalada polisi na
mamlaka hiyo itasaidia kuwafuatilia wahusika na kuwafikisha mbele ya
vyombo vya sheria .
Alisema mitandao yote imesajiliwa hata kama aliyehusika kuchafua
anaishi uvunguni atakamatwa kwa kuwa mitandao haipo kwa ajili ya
matumizi yasiyo sahihi ambayo hayaruhusiwi.
Mtungahema, amesema atakaebainika anatumia mtandao kumchafua mtu
mwingine huyo amefanya kosa la jinai hivyo afikishwe mbele ya vyombo vya
sheria kwa kuwa tayari zipo sheria zinazotoa adhabu kwa mtuhumiwa
atakaepatikana na hatia.
Aliongeza kuwa TCRA, imeshapokea malalamiko mengi na tayari
wahusika wameshatiwa mbaloni na ufuatiliaji utaendelea ili mradi tu
mamlaka hiyo itaarifiwe .
Nchi wanachama wa jumuia afrika mashariki zimeaanza kikao cha siku
nne mjini Arusaha kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa chang moto
mbalimbali zinazoikabili sekta ya mawasiliano.
Mwenyekiti wa jumuia hiyo ya sekta za mawasiliano, EACO, Dakta
Fracis Wangusi, amesema sekta ya mawasiliano inakabilwa na changamoto
mbalimbali ambazo zinakwamisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa
haraka.
Wangusi ambae pia ni mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano
nchibni Kenya,amezitaja sekta hizo kuwa ni pamoja na kuhama kutoka
mtandao wa analojia kwenda digital na matumizi ya visumbusi kwa ajili
ya luninga.
Aliongeza kuwa , sekta ya simu inakabiliwa na changamoto ya kuwepo
gharama kubwa za matumizi ya simu, usambazaji barua na vifurushi
kunakofanywa namashirika ya posta unaotokana na ukuaji wa mji ambao
haujapangiliwa ,matumizi ya vikwazo vya kuchelewesha huduma ya haraka
ya internet .
Alisisitiza kuwa ili kupatikana kwa mafanikio hayo ni kuondoa vikwazo na kuhimiza uwekezaji kwenye sekta ya mawasiliano ICT.
Related
TEKNOLOJIA: JIFUNZE JINSI YA KUTENGENEZA WINDOWS BOOTABLE FLASH (KISWAHILI & PICHA)
Nimekutana na hili swali kwa muda mrefu sasa na ili kuonesha mapenzi yangu ya dhati kwa mafans wangu, leo nakuja na jinsi ya kutengeneza Bootable flash kwa ajili ya kupiga window kwa lugha ya ki...
TECHNOLOJIA: JIFUNZE JINSI YA KU 'UNLOCK' MODEM YAKO. (KISWAHILI)
Inawezekana umejiuliza kwa mara nyingi ni jinsi gani unaweza kutumia line za mitandao yote katika modem yako bila kupata jibu. Usijali, leo Jarida Huru inakupa uwezo wa kujifungulia modem yako b...
Older Post
JH STORY: KISA CHA BINTI MARIAMU
Post a Comment

:noprob:

:smile:

:shy:

:trope:

:sneered:

:happy:

:escort:

:rapt:

:love:

:heart:

:angry:

:hate:

:sad:

:sigh:

:disappointed:

:cry:

:fear:

:surprise:

:unbelieve:

:shit:

:like:

:dislike:

:clap:

:cuff:

:fist:

:ok:

:file:

:link:

:place:

:contact:
Tabs
Za JuuMitandaoPiga Kura
Za Juu
-
Mmoja wa waasisi wa mtandao wa kijamii wa Instagram, amesema kuwa sheria zake kuhusu picha za uchi hazimbagui mtu yeyote. Kampuni hi...
-
Dar es Salaam. Harakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 zimeanza. Polisi wameanza mafunzo yatakayowaongezea uwezo wa kusimamia uchagu...
-
AMA kweli kufa kufaana! Lile bifu zito lililokuwa likitokota kati ya wapendwa wawili, Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu na mwi...








