BURUDANI: MSIBA WA 'TYSON' WAWARUDISHIA WEMA NA KAJALA USWAHIBA, WAKALISHWA KIKAO CHA SIRI

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/burudani-msiba-wa-tyson-wawarudishia.html
AMA kweli kufa kufaana! Lile bifu zito lililokuwa likitokota kati ya wapendwa wawili, Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu na mwigizaji mwenzake wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja limekwisha kufuatia kukalishwa katika kikao cha siri kilichofanyika kwenye msiba wa aliyekuwa mwogoza filamu mahiri nchini, marehemu George Otieno ‘Tyson’, Risasi Mchanganyiko limeinasa.