
Liverpool inajianda kwa msimu mpya wa ligi ya Uingereza
Mshambulizi wa Liverpool Dejan
Lovren aliifungia the Reds bao lake la kwanza katika mechi yake ya
kwanza Liverpool ilipoilaza Borussia Dortmund mabao 4-0 katika mechi
ya kirafiki.
Daniel Sturridge ndiye aliyeifungua kivuno hicho cha mabao baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Phillippe Coutinho.
Lovren, aliyejiunga na ''the Reds''
akitokea Southampton, katika kandarasi ya pauni milioni 20m alifuma bao
la pili kwa kichwa alipotumia vyema kona kutoka kwa Steven Gerrard .

Liverpool inajianda kwa msimu mpya wa ligi ya Uingereza
Jordan Henderson alikamilisha kivuno hicho baada ya kufaidi pasi ya Sturridge.
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers aliwachezesha
wachezaji wapya Lovren, Javier Manquillo, Emre Can Rickie Lambert
katika mechi hiyo.
Liverpool, itafungua kampeini ya msimu huu dhidi ya Southampton jumapili ijayo.

Kocha Rodgers aliwachezesha wachezaji wapya
Kwa upande wao Dortmund ilikuwa inatumia mechi
hiyo kujiandaa kwa mechi dhidi ya Bayern Munich ya kuwania kombe la
German Super Cup siku ya jumatano.
Dortmund itafungua kampeini yake dhidi ya Bayer Leverkusen tarehe 23 Agosti.