SOKA: TP MAZEMBE, SETIF ZATINGA HATUA ZA NUSU FAINALI KLABU BINGWA BARA LA AFRIKA

Setif, ambao walikuwa mabingwa wa Afrika mwaka 1988, walifahamu kuwa kwenda sare nyingine nyumbani, ilitosha kwao kufuzu wakiwa wamesalia na mechi moja kucheza.
Akram Djahnit aliingiza mabao mawili ya Setif yaliyo wawezesha klabu hiyo kusonga mbele kwa kupata pointi waliyoihitaji mno.
Setif inashikilia nafasi ya pili katika kundi B kwa alama 9, alama moja nyuma ya CS Sfaxien waliopata nafasi hiyo mnamo siku ya Ijumaa baada ya kushinda Al Ahli Benghazi ya Libya kwa bao moja bila.