jaridahuru

Mitandao

BURUDANI: SERENGETI FIESTA YAANZA KWA KISHINDO MJINI MWANZA, DIAMOND AFANYA KUFURU JUKWAANI (PICHA)

Msanii wa Bongo Flava, Linah Sanga (wa pili kushoto) na mkali wa muziki huo na mshindi wa tuzo ya AFRIMMA 2014, Diamond Platinum (kushoto) wakifanya vitu vyao katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana.
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platinum' (kushoto), akilitawala jukwaa pamoja na baadhi ya wacheza shoo wake katika onyesho la kwanza la Tamasha la Serengeti Fiesta katika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza jana jioni. Serengeti Fiesta inadhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Young D, akifanya vitu vyake ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba, jana wakati wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2014, lilipofanyika kwa mara ya kwanza mjini Mwanza jana.
Msanii wa Bongo Fleva, Mr Blue akikonga nyoyo za umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza waliojitokeza katika Uwanja wa CCM Kirumba katika Tamasha la Serengeti Fiesta.
Wasanii wa kikundi cha Makamandoo wakiwa kazini wakati wa Tamasha la Serengeti Fiesta la mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza jana.
Meneja wa Bia ya Serengeti, Rodney Rugambo (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba wakati wa tamasha hilo.
Wasanii wa kundi la Tanikando Group kutoka Igoma, Mwanza nao wakionyesha umahiri wao kupamba onyesho la muziki la Serengeti fiesta uwanjani hapo jana.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakishangilia baada ya kukongwa na burudani wakati wa Tamasha la Serengeri Fiesta lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana. Maonyesho hayo yatafanyika katika mikoa 18 nchini

Related

Michezo 6414657579313009820

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item