WORLDCUP: HATIMAYE CAMEROON WAKUBALI KUKWEA PIPA KUELEKEA BRAZIL, NI BAADA YA KUONGEZEWA POSHO
Wachezaji hao walikuwa wakilalamikia kiwango cha fedha £61,000 ambazo walikuwa wamepangiwa kupewa wakisema hazingetosha.
Haijabainika vyema ni kiasi gani walichoongezewa ndio wakakubali safari.
Hata hivyo rais wa shirikisho la soka la Cameroon Bw.Joseph Owona amesema 'baada ya kuweka kila kitu wazi ,mzozo huo umetatuliwa na sasa hamna tatizo'.
Tatizo lililopo sasa kwa masimba hao ni kupata mkakati madhubuti wa kukabiliana vilivyo na timu za kundi lao A ambamo wamo miamba ya soka wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.







































