KIMATAIFA: BOKO HARAM WAENDELEA KUITESA NIGERIA, WAWATEKA WANAWAKE 20 NA WANAUME 3 KWA MARA NYINGINE

Mlinzi mmoja wa kijiji alisema kuwa washambulizi hao pia waliwateka nyara wanaume watatu waliojaribu kuwazuia wasiondoke na wanawake hao.
Hadi sasa jeshi halijasema lo lote kuhusiana na tukio hilo.
Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Chibok ambako wapiganaji wengine wa silaha waliwteka nyara zaidi ya wasichana 200 wanafunzi Aprili, mwaka huu.
Wakati huo jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaua wapiganaji 50 katika kampeni yake dhidi ya magaidi mwishoni mwa wiki katika majimbo la Borno na Aladawa.
Mfululizo wa mashambulizi Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo umeimarisha ukosoaji wa vyombo vya usalama vya Serikali.
Licha ya kuwepo kwa hali ya hatari katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wanajeshi hawajachukua hatua dhabiti na wakati mwingine hawapo wakati washambulizi wanaotekeleza uhalifu wao