jaridahuru

Mitandao

ELIMU: WAKUU WA SHULE ZILIZOBORONGA FORM SIX 2014 WAKIWEMO WA TAMBAZA NA IYUNGA WAPEWA MWEZI KUJIELEZA

Wakuu wa shule za serikali zilizofanya vibaya kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu  pamoja na Maofisa elimu wa Mikoa wamepewa muda wa mwezi mmoja ili kubaini chanzo cha  shule zao kuwa na ufaulu hafifu.
 Baada ya kubaini chanzo hicho cha ufaulu hafifu wanatakiwa kutoa taarifa kwa katibu mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa-TAMISEMI.
 Miongoni mwa shule ambazo wakuu wake wametakiwa kujieleza ni pamoja na shule ya Tambaza iliyopo jijini Dar es salaam na shule ya Iyunga ya Mkoani Mbeya, ambapo muda huo wa mwezi mmoja umeanza  leo.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam,  katibu Mkuu Tamisemi Jumanne Sagini amesema, kushuka kwa ufaulu kwa shule hizo kumewashtua  watu wengi, kwani shule hizo zimejengewa uwezo mzuri wa vifaa pamoja na miundombinu.
 
Hata hivyo Sagini amesema, idadi ya wanafunzi 22,685 waliofaulu masomo ya sayansi kwa mwaka  huu wa 2014  ni kubwa kwa  zaidi ya wanafunzi 3,939 ikilinganishwa na wanafunzi 18,746  waliofaulu masomo hayo mwaka jana.
 
Amesema kuwa ufaulu huo umeipa changamoto Serikali na imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi ambae amefaulu na kupata alama stahiki  katika masomo aliyoyachagua anapata shule.
 
Aidha amewataka wazazi wa wanafunzi waliokuwa wamepangiwa kusoma masomo ya sanaa ilihali ufaulu wao ni katika masomo ya sayansi, kutokuwa na wasiwasi kwani serikali imebaini changamoto hiyo na kuifanyia kazi.

Related

JAMII: MGANGA WA KIENYEJI AMKATA MTOTO SEHEMU ZA SIRI NA KUZIPIKA HUKO MAGU

Bukoba. Polisi wanamshikilia mganga wa jadi kutoka Kijiji cha Matera, Kata ya Nyanguge, Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza kwa tuhuma za kumnyonga mwanafunzi wa darasa la kwanza, Fausta Geofrey ...

KITAIFA: VIONGOZI 6 WA VIKUNDI VYA MBWA MWITU NA PANYA ROAD WATIWA MBARONI

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata viongozi sita wa makundi ya uhalifu maarufu kwa majina ya Mbwa Mwitu na Panya Road. Akizungumza na waandishi wa habari jij...

TEKNOLOJIA: FACEBOOK YAMUOKOA MKWEZI TOKA FUTI 80 YA MLIMA ALIKOPOTEA

Mkwezi wa milima mirefu ameokolewa kutoka futi 80 bondeni alipoandika ''Nahitaji msaada'' katika mtandao wa Facebook John All aliyeokolewa Profesa huyo wa jiografia aliwaambia marafiki zake...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item