jaridahuru

Mitandao

KITAIFA: VIONGOZI 6 WA VIKUNDI VYA MBWA MWITU NA PANYA ROAD WATIWA MBARONI



JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata viongozi sita wa makundi ya uhalifu maarufu kwa majina ya Mbwa Mwitu na Panya Road.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova, aliwataja viongozi hao kuwa ni Athumani Said (20), Joseph Ponela, Clement Petter (25) na Romans Vitus (18) wakazi wa Kigogo.

Wengine ni Mwinshehe Adamu (37) mkazi wa Temeke na Daniel Petter (25) mkazi wa Yombo, huku kamanda huyo akibainisha kwamba maeneo yenye vijana hao wahalifu ni Kigogo, Magomeni, Tabata, Manzese na Mbagala ambapo askari wa kutosha wapo kwa lengo la kuwadhibiti.

Kova aliwaonya wanaoeneza uzushi kwamba makundi hayo ya wahalifu yamevamia maeneo hayo jambo alilodai kuwakosesha wananchi amani huku akisisitiza kuwa si kweli.

Alisema uchunguzi wa jeshi hilo umebaini kwamba chanzo cha uvumi huo ni baada ya mauaji ya vibaka wawili walihusishwa na makundi hayo yaliyotokea Mei 18 na Mei 20 mwaka huu eneo la Kigogo Sambusa.

Related

Kitaifa 5770243107634376607

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item