jaridahuru

Mitandao

AFYA: EBOLA YAZIDI KUINYEMELEA AFRIKA MASHARIKI, FAHAMU JINSI YA KUJIKINGA NA EBOLA NA MADHARA YAKE

Mgonjwa wa EBOLA

Ebola ni ugonjwa hatari unaosababishwa na kirusi kiitwacho ebola. Kirusi hicho ni moja kati ya familia ya virusi watatu toka katika familia ya filoviridiae.

Zipo aina tano za kirusi cha ebola ambao nao ni bundibugyo ebolavirus (BDBV), zaire ebolavirus (EBOV), reston ebolavirus (RESTV), sudan ebolavirus (SUDV) na tai forest ebolavirus (TAFV).
Aina hizo tatu za virusi, yaani BDBV, EBOV na RESTV, ndiyo inayongoza kwa kusababisha mlipuko wa ugonjwa huo barani Afrika. Wengine wanapatikana nchi za Asia, yaani Ufilipino na Thailand na mpaka sasa hakuna taarifa za kusababisha vifo.

Kwa mara ya kwanza ugonjwa huu uliripotiwa kutokea mwaka 1976 katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hatari ya mgojwa kupoteza maisha ni asilimia 90. Watu ambao wako katika hatari ya kupata ugonjwa huo ni jamii inayoishi karibu na jamii ya wanyama au watu walioathirika.
Pia uwepo katika mazishi ya wagonjwa wa ebola wakati wa shughuli za kuzika na kugusana na majimaji ya mgonjwa aliyekufa.

Unavyoambukizwa na kuenea
Chanzo cha ugonjwa katika makundi yetu ni mtu mmojawapo kugusana na damu au majimaji ya wanyama waliombukizwa, ambao mara nyingi ni nyani, sokwe, tumbili na popo. Inaaminika kuwa popo wanaopenda kula matunda, wanaeneza ugonjwa huo bila wao kuaathirika.
Katika jamii yetu ugonjwa huu huweza kuambukizwa kutoka mtu mmoja mwenye maambukizi kwenda kwa mwingine baada ya kugusana na damu au maji maji kupitia michubuko au majeraha juu ya ngozi.

Watu walio na maambukizi na wakapata nafuu bado wanaweza kuwaambukiza wengine kwa zaidi ya miezi miwili, pia wanaweza kuwambukiza watu wengine kwa njia ya kujamiana.

Dalili za ugonjwa
Jina jingine la ugonjwa huu ni ‘ugonjwa wa kuvuja damu’. Hii ilitokana kujitokeza dalili ya kuvuja damu mwilini.

Dalili za ugonjwa huu huu huanza kujitokeza kuanzia wiki ya pili au ya tatu tangu kugusana na damu au majimaji ya mwilini ya mgonjwa wa ebola.

Dalili zake ni homa kali, maumivu ya koo na misuli, kichwa kuumwa na mwili kuwa dhaifu.
Baadaye dalili zingine hujitokeza baada ya ini na figo kuanza kuathirika dalili hizo ni kama kuhisi kichefu chefu, kutapika na kuharisha.

Uchunguzi na matibabu
Sampuli ya damu ya mgonjwa hupimwa ili kutambua askari mwili maalumu walizalishwa na mwili kupambana dhidi ya virusi ebola. Pia kutazama uwepo wa DNA ya virusi wenyewe.

Ugonjwa huu hauna tiba wala chanjo kama ilivyo kwa magonjwa mengi yanayosababishwa na virusi ambayo huwa hayana dawa wala chanjo, bali ni matibabu ya kumsaidia mgonjwa kupata ahueni ambayo ni kama vile kuongezewa maji kwa njia ya mshipa.

Mpaka sasa hakuna kampuni wala hospitali iliyopewa leseni ya kuuza au kutengeza chanjo.
Kujikinga na kuudhibiti ugonjwa wa ebola

Ugonjwa huu unaweza kuzuia kujitokeza na kupunguza kuenea kwa kuwachunguza wanyama walio na ugonjwa na kuwaua na kisha kuyatupa mabaki yao.

Kuhakikisha nyama zinapikwa vizuri, kuvaa mavazi maalumu ya kujikinga kwa wale wanaofanya shughuli za wanyama pamoja na watoa huduma za afya
 
Related

Jamii 6303385025957673418

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item