jaridahuru

Mitandao

JH STORY: KISA CHA BINTI MARIAMU




Binti Mariamu
Weekend hii kwangu ilikuwa ya tafakuri nyingi zisizo na majibu na msongo mkubwa wa mawazo. Ilikuwa weekend yenye kuumiza na ya kujiuliza sana juu ya mustakabali wa maisha yangu ya mahusiano.

Nilienda kwenye send off ya mchumba wa kaka yangu.

Moshi, Kilimanjaro 1994

Baba alikuwa amehamishiwa mkoa wa Kilimanjaro kama Mkuu wa Polisi Wilaya ya Moshi Mjini. Mwaka huo huo alikuja Afisa Mifugo mpya wa Wilaya. Tulikuwa tukiishi karibu maeneo ya Shanty Town. Afisa mifugo huyu alikuwa na watoto watatu. Wa kwanza ni binti mkubwa (dada Pendo), wa pili ni binti mwingine mrembo zaidi (Mary) na mdogo wao wa kiume (Michael).

Nilikuwa naingia darasa la nne.

Dada Pendo alikuwa anaingia darasa la sita na Mary ndo alikuja kuanza darasa la Kwanza wakati Michael alikuwa bado mdogo kuanza shule ya msingi hivyo yeye alienda shule ya awali ya St. Margeth maeneo ya kule kule shanty town.
Pendo, Mimi na Mary tulienda shule moja ya Kibo primary enzi hizo mwalimu mkuu ni mama Nkya.

Tulipatana sana na Mary kwani licha ya kucheza pamoja nlikuwa nikimfundisha sana hesabu. Na kwa vile tulikuwa majirani basi tulishirikiana kwa mambo mengi…hadi nilipomaliza shule ya msingi tulikuwa na urafiki mkubwa sana.

Sekondari nilipangiwa Kibaha na hata huko bado niliendelea kuwasiliana na Mary. Tuliwasiliana zaidi kama marafiki na kwa kipindi kile hakuna kati yetu aliyekuwa akiwaza mapenzi (atleast kwangu sikuwa nikiwaza kabisa).

Dada yake na ndugu wengine walifahamu jinsi tulivyokuwa tunapatana na Mary hadi wazazi wake wakawa wanatuita wachumba.

Mary ni binti aliyelelewa vizuri kwao. Nashindwa kuamua nimeliona hilo zaidi kwake kwa kuwa tu tulikuwa majirani au ni kweli ni mmoja wa mabinti waliofunzwa wakafundika.

Mary ameniona at my best and worst moments..na katika nyakati zote hizo bado tuliendelea kuwa marafiki.

Nakumbuka utotoni nilikuwa nikitoroka nyumbani kwenda kucheza mpira uwanja wa Ushirika. Siku moja nilirudi usiku baba akanichapa nje ya nyumba yetu huku Mary akiniona. Of course pamoja na kuona aibu sikuacha kutoroka, ila siku mbili baadaye nilirudi nyumbani jioni. Mary aliponiona tu akanikimbilia akanipeleka kwao nkanawa miguu halafu kama nusu saa hivi nikatoka nje na yeye akaniaga kwa nguvu ili wajue nlikuwa kwao namfundisha…

December, 2009

Baada ya kumaliza chuo tuliendelea sana kuwasiliana na Mary. Wakati huu mawasiliano yetu yalibadilika kwenda more personal. Kwa bahati nzuri she was as single as I was. Tukawa tunawasiliana sana..calls. sms na safari za mara kwa mara kwenda Arusha ambako ndiko aliko kwa sasa.

Ghafla mwaka 2010..

Mary akanitext kuniambia kuwa kuna kitu kinaendelea kwa dada yake. Kwanza dada yake alimuambia kuwa amepata boyfriend ila hata yeye mwenyewe Mary atakuwa anamfahamu sana tu. Hakuhisi chochote hadi aliponitumia ujumbe huo mfupi. Alikuwa ni kaka yangu.

Sijui ni lini walianza mahusiano yao lakini kwa vyovyote vile walijua mimi na Mary tulikuwa more than friends. Ni mara nyingi nilikuwa namuambia bro naenda Arusha kumsalimia Mary. Kwani yeye alidhani nilikuwa naenda kucheza naye karata? Au kuruka kamba? <machungu> Ndiyo sikumuambia exactly uhusiano wetu ulipofika ila ni kwa sababu haukuwa muda muafaka.

Kaka yangu akanizunguka akaenda kumchumbia dada Pendo.

Nakumbuka Mwaka juzi nilipoenda tena Arusha Mary alitaka nimpe mimba tu lolote na liwe alimradi tu tuvunje mipango yao. Alinisisitiza sana ila nilimkatalia…how I wish I just did it <majuto>.

Muda ulienda haraka mara tukaitwa utambulisho wa shemeji yetu kama familia.

Ilikuwa kama miaka ile tulipokuwa tunaishi wote Moshi. With the exception ya mimi, watu wote walikuwa na furaha sana. Nilishindwa kujua kwa nini kaka yangu aliamua kunifitini vile <usaliti>.

Ghafla tukaenda kupeleka posa kwa kina Mary…mtoto mchanganyiko wa Kisukuma na Mnyakyusa..yaani mchangamfu ila adabu tele. Acha tu!!!!! <machungu>

I wish ningemkubalia Mary wazo lake kipindi kile..sasa Mary ni shemeji yangu.

Mary, kwa yeyote atakayekuja kukuoa..am sure amepata mke mwema. Sijaona binti mwenye nidhamu kama wewe. Mcheshi na mwenye kupenda watu.

Jumamosi hii ndiyo tulikuwa Morogoro, walipo wazazi wa Mary, kwenye send off party ya binti yao, dada Pendo, ambaye mwisho wa mwezi ujao atakuwa officially shemeji yangu and hence make Mary officially out of bounds for me.

Ndo nimerudi kutoka Morogoro jana..na sasa nipo kazini,


Wasalaam wapendwa,

Related

JH STORY: UTAOA LINI BWANA?!

UTAONA LINI... Normal 0 false false false EN-GB X-NONE X-NONE ...

JH STORY: NAOGOPA KU 'CHEAT' NISIJE UMIZWA

1999, Himo - Kilimanjaro Nilikuwa nimemaliza Chuo Kikuu cha Mlimani wanavyokiita watoto wa siku hizi. Enzi zetu ilikuwa ‘The University of Dar es salaam’ na heshima zote kijijini mtoto ...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item