KIMATAIFA: KUNDI LA AL-SHABAAB WATOA AMRI, WATAKA WANAWAKE WAVAE Niqab

Hawakuadhibiwa kwa sababu lilikuwa kosa lao la kwanza lakini walionywa kuwa watachapwa hadharani ikiwa wangepatikana na kosa hilo kwa mara nyingine.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa wanawake hao walivalia mavazi mapesi na kukosa kujifunika nyuso zao kutokana na joto kali.
Wanawake hao waliamrishwa kuvaa Niqab,vazi linalowafunika mwili mzima huku sehemu ndogo ya uso ikiachwa nje ili kuwawezesha kuona.
Jina al shabaab linalo maanisha "vijana" kwa kiarabu,linapigania mfumo wa kiislamu wa wahhabi saudia.
Watu ambao washawahi kupatikana na kosa la Zinaa wamepigwa mawe hadi kufa na wezi kukatwa mikono.
Serikali ya Somalia inayofadhiliwa na umoja wa mataifa,ikisaidiwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika, imefaulu kutimua Al-shabaab nje ya miji mikubwa nchini humo lakini kundi hilo bado linaendelea kutekeleza mashambulizi huko.