KIMATAIFA: KITUO CHA NTV UGANDA KIMEFUNGIWA BAADA YA KUMUONESHA MUSEVENI AKIWA AMESINZIA BUNGENI

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/kimataifa-kituo-cha-mtv-uganda.html
Serikali
ya Uganda imekifungia kituo kikubwa cha Televisheni cha nchi hiyo NTV
kuripoti habari zozote zinazomhusu Rais baada ya kurusha hewani picha
zinazomuonyesha Rais Yoweri Museveni amesinzia bungeni.
Mkurugenzi wa kituo cha habari za serikali Dennis Katungi amenukuliwa akisema: “Rais ana tabia zake wengi mnajua, huwa anatafakari na wanajua lakini bado wameonyesha picha hizo na kusema alikuwa amesinzia.”
Msemaji
wa serikali Ofwono Opondo amethibitisha kuwa NTV Uganda itachukuliwa
hatua za kinidhamu ambapo wameifungia kuripoti habari zozote zinazomhusu
rais wakati bado serikali ikiangalia uhusiano wake na chombo hicho.
Ameituhumu
NTV kwa kukosa utaalamu wa uandishi na kuegemea upande mmoja lakini
hata hivyo hatua hiyo si ya kudumu ni ya muda tu kuwafanya wafikirie
upya.