KIMATAIFA: WAPIGANAJI WA JIHAD WAENDELEA KUTEKA MIJI ZAIDI
Wapiganaji hao vilevile wameiteka miji zaidi katika mkoa wa Anbar ambapo mwandishi huyo anasema kuwa lengo lao ni kuitumia kuvamia mji mkuu wa Baghdad.
Waasi hao wanasema kuwa waliiteka miji hiyo bila kumwaga damu kupitia majadiliano na makabila ya kisunni.
Wanamgambo wa Kishia hapo jana walifanya gwaride mjini Baghdad, na kuzua wasiwasi kuhusu tofauti inayozidi kuibuka kati ya watu wa dhehebu la kishia na wale wa Kisunni.







































