MICHEZO: SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF) LACHIMBA MKWARA MZITO, LAAHIDI KUTOFUMBIA MACHO VITENDO VYA RUSHWA
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/08/michezo-shirikisho-la-soka-tanzania-tff.html
Dar es Salaam. Wakati pazia la usajili likifungwa leo, Bodi ya Ligi kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesisitiza kuwafungia wote watakaohusika na vitendo vya rushwa.
Mkurugenzi mpya wa mashindano, Boniface Wambura
aliliambia gazeti hili kuwa TFF haitafumbia macho vitendo hivyo na
kuwataka wachezaji na waamuzi kutojihusisha na vitendo hivyo.
“Kwa sasa awe kiongozi, mchezaji au mwamuzi
atakayepatikana amejihusisha na vitendo vya rushwa au kupanga matokeo
katika mchezo na ikabainika, tutamfungia maisha kujishughulisha na
mpira.
“Hatutamwonea mtu lakini pia hatutampendelea mtu.
Ndio maana kabla ya ligi tumekuwa tukijitahidi kutoa semina na kozi
maalumu kwa waamuzi, ligi hii hatutakuwa na huruma na mtu,” alisisitiza
Wambura.
Mechi mbalimbali za mpira wa miguu nchini,
zinachezewa kwenye kamari kubwa kwa kununua mechi hizo kwa dau kubwa
kabla ya mechi haijachezwa.
“Wachezaji na waamuzi waepuke kupanga matokeo ya
mechi kwa ahadi za kupewa chochote kwenye mechi. Kufanya hivyo ni
kudumaza soka nchini,” alisema. Hivi karibuni, rais wa TFF, Jamal
Malinzi alisema kuwa zaidi ya waamuzi watatu wenye beji ya Fifa
wamesimamishwa kuchezesha soka ndani na nje ya nchi kwa sababu ya
kupanga matokea ya mechi. Alisema hadi sasa Fifa wanaendelea na
uchunguzi wa tuhuma hizo na kuahidi adhabu kali kwa watakaobainika.