ELIMU: KERO YA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI KUKATISHWA MASOMO YAPATIWA MUAROBAINI WAKE
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/08/elimu-kero-ya-wanafunzi-shule-za-msingi.html
Kutokana na changamoto hiyo akiwa wilayani Mvomero mkoani Morogoro katika ziara yake Rais Jakaya Kikwete amewaagiza viongozi wa mkoa wa Morogoro kutafuta majibu ya kumaliza tatizo la wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza kushindwa na kumaliza elimu ya sekondari.
Rais Kikwete ameongeza kwamba lengo la serikali ni kutengeneza taifa la wasomi lakini inashangaza kuona kwa wilaya ya Mvomero zaidi ya asilimia 58 ya wanafunzi waliojiunga na kidato chaa kwanza miaka minne iliopita wameshindwa kumaliza elimu ya sekondari kutokana na sababu mbalimbali na kuagiza viongozi kushughulikia tatizo hilo.
Kwa upande mwingine Dr Kikwete akiwa wilayani Gairo amepata fursa ya kutembelea mradi wa maji ambao unafadhiliwa na benki ya dunia kwa gharama ya shilingi bilioni 6.6 pia amezindua chumba cha upasuaji ambacho kimegharimu shilingi milioni 82.