BIASHARA: MAANDALIZI YA BIDHAA CHANGAMOTO KUBWA KWA WAJASIRIAMALI NCHINI

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw Mlowe amesema katika mafunzo hayo yaliyofanyika jana na leo jijini Mwanza yamepata mafanikio makubwa kwa kuwepo kwa mwitikio kwa wajasiriamali wakiume zaidi ya wanawake.
Aidha pamoja na mwitikio mkubwa kutoka kwa wajasiriamali amebaini kutokuwepo kwa elimu ya kutosha kwa wahusika wa mafunzo hayo hasa kwenye maandalizi ya bidhaa.
Mafunzo hayo yalishirikisha wajasiriliamali ambao wanajihusisha na uuzaji wa asali, maembe, chili, pilipili na bidhaa nyingine mbalimbali ambazo zimekuwa zikiuzwa katika soko la ndani ila la nje hazipatikani.
Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa asasi, taasisi na mashirika mengine ambayo yanajihusisha na kuelimisha kutoa elimu ya jinsi ya kuandaa bidhaa hasa katika kuweka lebo ili kuhakikisha kuwa ubora wanajitokeza katika kutoa elimu ili bidhaa za wajasiriamlai ziwe na ubora unaotakiwa kimataifa