RUVUMA: ASKARI POLISI MBARONI KWA KUMPIGA RISASI DEREVA BODABODA MKOANI RUVUMA

Aidha risasi hizo zimemjeruhi kwenye kiganja cha kushoto na paja la kushoto ambapo risasi ya tatu ilnasa kwenye simu ya kiganjani. Askari huyo alifanya tukio hilo kufuatia kutoelewana baina yake na Mwendesha Bodaboda huyo.
Kwa upande mwingine kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo Msikhela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema askari wawili waliohusika na tukio hilo wamewekwa mahabusu na hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao uchunguzi utakapokamilika.