jaridahuru

Mitandao

HISTORIA YA MWANAHARAKATI STEVE BIKO


Tukizungumzia mwanaharakati wa haki za watu weusi wengi wanajua bishop desmond tutu, Nelson Mandela, Winnie Mandela na wengine wengi ambao walishiriki katika harakati za ukombozi wa watu weusi nchini afrika kusini.

Leo nataka umjue mwanaharakati aliechangia kwa kiasi kikubwa katika kuanzisha harakati za kupigania haki za watu weusi nae si mwingine bali ni Steve Bantu Biko.
Steve Biko alikuwa akifahamika kama mwanaharakati anayepiga vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, mnamo miaka ya 1960 na 1970.
Biko alikuwa kiongozi wa wanafunzi, baadae akaanzisha vuguvugu la Black Consciouness Movement.

Vuguvugu hili lilipata nguvu sana na kuenea karibuni katika miji mingi yenye idadi kubwa ya watu weusi.
Mauti yalimfikia baada ya kutiwa mbaroni na kuteswa na maaskari wa serikali ya kibaguzi. Biko alijulikana kama jabali la harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Wakati yupo hai, alikuwa akiandika sana masuala ya harakati za kujaribu kuwatia nguvu watu weusi na aliweza kuwa maarufu kwa wito wake wa kusema kwamba “black is beautiful” akimaanisha kwamba “mtu mweusi ni mzuri.”

Alielezea maana ya msemo huu ni: “mtu, ni sawa kama ulivyo mtu, lakini anza kujiangalia mwenye ukiwa kama binaadamu.
Stephen Bantu Biko alizaliwa mjini King Williams Town, ndani ya jimbo la Eastern Cape nchini Afrika Kusini. Biko alikuwa mwananfunzi wa Chuo Kikuu cha Natal Medical School.
Hapo awali Biko alikuwa akijishughulisha na masuala ya kutafuta “Umoja wa Umma wa Wanafunzi Afrika Kusini”.

baada ya kuweza kuwaadikisha watu weusi, wahindi, na watu weupe pia, kwamba wakiwa kama wanafunzi wanahitaji jumuiya itakayokuwa inawaangalia wanafunzi.
Kwa mpango huo aliweza kufanikisha kuanzishwa kwa Jumuiya ya Wanafunzi nchini Afrika ya Kusini, kwa Kiingereza: South African Students’ Organisation mnamo miaka ya 1968, na Biko akachaguliwa kuwa kama rais wa kwanza wa juimuiya hiyo.
SASO pia ilikuwa na mahusiano ya kisiri na jumuiya ya Harakati za kujitambua kwa watu weusi. Mke wa Biko Ntsiki Mashalaba, alikuwa mchangiaji mzuri wa kundeleza jumuiya ya “Harakati za kujitambua kwa watu weusi”.

Mnamo mwaka 1972 Biko akawa rais wa kuzuga kuwa ndio rais anaeangalia kanuni za watu weusi .
Biko aliwekewa vikwazo wakati wa kipindi cha ubaguzi wa rangi umeshamiri mnamo Machi mwaka 1973. Lengo kuu la kumvisha kiremba cha ukoka bwana Biko, walimaansha ya kwamba Biko haruhusiwi kuzungumza na zaidi ya mtu mmjoa kwa wakati mmoja.

Biko aliwekewa hadi mipaka katika baadhi ya sehemu asikanyage kabisa yaani.
Pia hakuruhusiwa kuzungumza mbele ya hadhara. Vile vile ilikatazwa kabisaa kuzungumzia dondoo za Biko alizokuwa akisema, ikiwemo tamko au maneno yoyote yale azumngumzayo bwana Biko.
Wakati Biko wamemuwekea vikwazo, harakati zake za kinchi zilizuiliwa katika jimbo la Eastern Cape, mahali alipozaliwa Biko.

Baada ya Biko kurudi kule kwao alikozaliwa, akaanzisha tena jamii fulani iliyokuwa inaitwa “Jamii shinani” iliyoegemea hasa katika kutaka watu kujitegemea wenyewe , jumuiya ilibeba taasis mbambali ikiwemo, community clinic, Zanempilo, the Zimele Trust Fund (ambaye baadae ilitoa msaada kwa familia yake wakati Biko alivyofungwa kisiasa), Njwaxa Leather-Works Project na Ginsberg Education Fund.

Related

Life Style 729910121174802427

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item