jaridahuru

Mitandao

JAMII: DAKTARI HOSPITALI YA AMANA AIBUA SIRI KESI YA MBASHA, KESI HIYO YAPATA MASHAHIDI WANNE




KESI ya kubaka inayomkabili mume wa mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha (32), inatarajiwa kusikilizwa Agosti 22, mwaka huu, baada ya upelelezi kukamilika..

Hatua hiyo inakuja baada ya mshitakiwa huyo jana kusomewa maelezo ya awali ya kesi hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.

Akimsomea maelezo hayo jana mbele ya Hakimu Wilberforce Luago, Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai Mei 23 mwaka huu, eneo la Tabata-Kimanga, mshitakiwa alimbaka shemeji yake wakati mkewe, Flora akiwa hayupo nyumbani.

Mbasha, alikiri siku hiyo mkewe kutokuwapo nyumbani, lakini hakumbaka shemeji yake kama inavyodaiwa.

Wakili huyo wa serikali, alidai Mei 25, mwaka huu,  Mbasha alimbaka tena shemeji yake ndani ya gari, wakati wanakwenda kumtafuta Flora alipo, tuhuma ambazo alizikana pia.

Alidai siku hiyo hiyo, binti huyo alikwenda kutoa taarifa polisi na kupewa PF 3 na kwenda Hospitali ya Amana; kwamba daktari alithibitisha binti huyo aliingiliwa kimwili.

Baada ya Katuga kusoma maelezo ya awali, aliiambia mahakama kuwa watakuwa na mashahidi wanne.

Related

Jamii 3509079729056654847

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item