jaridahuru

Mitandao

VYUONI: WANAFUNZI CHUO CHA TUMAINI IRINGA WAGOMA, WADAI KUPEWA PESA YA KUJIKIMU


Wanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini cha Iringa vitivo vyote wamegoma kuingia madarasani kuushinikiza uongozi wa chuo hicho kutafuta njia mbadala ya kuwapatia fedha za kujikimu na chakula pindi wakisubiri fedha za mkopo kutoka bodi ya mikopo ambazo zimechelewa kutolewa.

Wanafunzi hao wamesema hali yao ni mbaya na hawezi kusoma kutokana na mazingira waliyonayo kwa sasa kwani hata chakula kukipata kwao imekuwa ni changamoto kubwa.

Tatizo la uchelewesha wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu limekuwa likilalamikiwa mara kwa mara hali ambayo hupelekea kuibuka kwa migomo na maandamano ya wanafunzi katika vyuo mbalimbali hapa nchini.

Wanafunzi hao wa chuo cha Iringa wameshindwa kuvumilia hali hii na kugoma kuingia madarasani huku wakisema maisha wanayoishi kwa sasa sio rafiki kwa masomo kutokana na ukosefu wa fedha hizo.

Waziri wa Mikopo wa serikali ya wanafunzi, Laraha Laizer amekiri kuwepo na mgomo lakini alisema mgomo huo sio halali kutokana na kukosa kibali cha kufanya maandamano hadi ofisi ya mkuu wa mkoa kupeleka malalamiko yao.

Alisema kuwa wanafunzi wa fani zote wamegoma kuingia madarasani tangu asubuhi kushinkiza bodi ya mikopo iwalipe hela ya kujikimu (meals and accommodation fees).

Alisema kawaida bodi ya mikopo huwa inatoa fedha za kujikimu mara mbili kwa muhula  (semester) ambapo ni kiasi kinachotolea ni 472, 000/= kwa kila mwanafunzi anayopata mkopo kutoka bodi ya mikopo, lakini tangu tarehe 03.04.2014 bodi haijawalipa fedha za kujikimu.

Kitu kingine wanachogomea wanafunzi hao pamoja na mambo  mengine ni uongozi wa chuo kuwakata shilingi laki moja na nusu kwa ajili ya huduma ya intenati lakini huduma hiyo ni hewa.(White elephant)

“Kwa mfano, ukienda pale chumba cha kompyuta utakuta hakuna huduma yoyote ya intaneti na ya kuchapa wakati kila mwaka chuo kinakata hela kwa kila mwanafunzi,” alisema  waziri mikopo.

Akitoa  ufafanuzi, Afisa Mahusiano (PRO), Agnes Kitundu wa jambo hili alikiri kuwepo kwa mgoma wa wanafunzi kutaka kuandamana kwenda hadi kwa mkuu wa mkoa, lakini wamekosa kibali cha kufanya hivyo.

Hata hiyo afisa mahusiano huyo alisema bodi ya mikopo tayari wameshawaingizia pesa kwenye akaunti zao na kuwamba kusitisha mgomo wao. Hata hivyo mpaka tukwenda mtamboni wanafunzi hao walikuwa hawajaingia madarasani.

Related

Vyuoni 293914091200169703

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item