https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/elimu-wafungwa-magerezani-sasa-kupata.html
Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) akisaini kitabu cha
wageni mara alipowasilishwa katika ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete (kulia).

Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (wa pili kulia) na Makamu Mkuu
wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete (wa tatu)
wakisani hati za makubariano ya ushirikiano kati ya Taasisi hizo mbili.
Wakwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini
Dkt Juma Malewa na wa nne kulia ni Naibu wa Tatu wa Makamu Mkuu wa Chuo
Prof. Modest Valisango anayeshughulikia Teknolojia na Huduma za
Kujifunzia Chuoni hapo.

Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Malewa(wa
kwanza kulia) na Prof. Modest Valisango (wa kwanza kushoto) wakisaini
hati za makubaliano ya ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Chuo
Kikuu Huria cha Tanzania.

Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja ( kulia) na Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete (
kushoto)wakibadilishana nyaraka muhimu za makubaliano ya ushirikiano
mara baada ya kutiwa sahini.

Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (wa pili kulia) akitoa maelezo
kwa waandishi wa habari juu ya undani wa ushirikiano kati ya Jeshi la
Magereza na Chuo Kikuu Huria.Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa, wa nne kulia ni Naibu
wa Tatu wa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Modest Valisango aliyepia Mkuu wa
Teknolojia na Huduma za Mafunzo chuoni hapo.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa
waandishi wa habari juu ya undani wa ushirikiano kati ya Jeshi la
Magereza na Chuo Kikuu Huria.Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa, wa nne kulia ni Naibu
wa Tatu wa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Modest Valisango aliyepia Mkuu wa
Teknolojia na Huduma za Mafunzo chuoni hapo.

Aliyewahi
kuwa mfungwa kwa takribani mika 20 gerezani Ukonga Ng. Haruna Pembe
(mwenye suti) akitoa ushuhuda wa jinsi alivyoweza kusoma na kumaliza
shahada yake ya sharia akiwa gerezani.Picha zote na Insp Deodatus
Kazinja, PHQ