SOKA-BONGO: JKT RUVU YAIBANA MBAVU MBEYA CITY, WATOA SULUHU YA BILA KUFUNGANA
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/09/soka-bongo-jkt-ruvu-yaibana-mbavu-mbeya.html
Wabishi wa jiji la Mbeya klabu ya Mbeta City leo imejikuta ikilegea kwa maafande wa JKT Ruvu baada ya kukubali kugawana ponti moja moja kwa kutoa sare ya 0-0 katika mchezo wa ufunguzi wa ligi uliopigwa kwenye uwanja wa Sokoine.
Mbeya City FC ambao mwaka jana walikuja na kasi ya ajabu na kujizolea mashabiki rukuki kutokana na umoja walio nao ikiwa pamoja na kujituma uwanjani huku wakiwa na hasira na timu kubwa kama Simba, Yanga na Azam FC msimu ulioisha mwaka jana walishika nafasi ya tatau na kuishusha Simba ambayo ilikamata nafasi ya nne nyuma ya Azam bingwa na makamu Yanga.
Kwa matokeo hayo ya bila kufungana yana fanya timu hizo mbili kugawana pointi 1 kila timu baada ya kushindwa kuchukua pointi 3 muhimu.