MAKALA / JAMII: FAHAMU JINSI FREEMASON ILIVYOINGIA TANZANIA, WAJUE VIONGOZI WAKWANZA NA MFUMO WA KIUTENDAJI
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/09/makala-jamii-fahamu-jinsi-freemason.html
Wiki iliyopita, mwandishi wa simulizi hizi, Kiongozi Mstaafu wa
Freemason Afrika Mashariki, Sir Andy Chande, alieleza namna Dikteta Idi
Amin alivyowatimua Freemason Uganda.
Hatua iliyosababisha jengo lililokuwa linatumika kugeuzwa kuwa kanisa.
Pia alieleza nanma watu wenye asili ya Afrika
Mashariki walivyochangamkia kujiunga na Freemason, kiasi cha kuanzisha
ofisi za watu weusi peke yao. Endelea...
Mwaka 1977 tulishuhudia Visiwa vya Ushelisheli
vikijiunga na Ofisi kuu ya Freemason Afrika Mashariki. Baada ya kusubiri
kwa muda mrefu, mwaka huo huo Septemba ilifunguliwa ofisi ya Freemason
ya Ushelisheli iliyopewa namba 8798 huko Victoria, mahe.
Mizizi ya Freemason katika Visiwa vya Ushelisheli
ilianza kukua mwanzoni wakati wa ujio wa mafundi kutoka Uingereza. Leo
Freemason imeendelea kupata nguvu na heshima katika kila kona ya visiwa
hivyo.
Hivi sasa wanachama wa Freemason katika visiwa hivyo wanaendelea kufanya kazi vizuri katika wilaya zote.
Ofisi ya kumi ya Freemason na isiyo na wanachama
wazungu ilifunguliwa Tanzania chini ya Mkuu wa Afrika Mashariki, jambo
lilitajwa kuwa ni la heshima, hasa ikikumbukwa historia ya Freemason
Afrika Mashariki.
Baadaye nilikuwa nikiitwa sehemu mbalimbali Afrika
Mashariki kwa ajili ya kuzindua ofisi mpya za Freemason, wakati huo
mbinu mpya zilikuwa zimeanza kutumika kuboresha huduma zetu.
Ofisi ya kwanza ya mwongozo ya Freemason
ilifunguliwa Nairobi nchini Kenya, chini ya Mkuu wa Ofisi hizo wa Afrika
Mashariki na kusimamiwa na ofisi ya Harmon namba 3084, iliyotumika kama
makao makuu kwa ofisi zote za Nairobi.
Baada ya kufunguliwa ofisi hiyo, haraka haraka
ikafunguliwa ofisi nyingine huko Kampala nchini Uganda. Ofisi hiyo
ilikuja kutumika kwa ajili ya eneo la bara la Afrika Mashariki.
Maendeleo hayo mapya yalikuja kuwa kichocheo
kikubwa cha maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwamo elimu. Mafanikio
hayo yalitajwa dhahiri kwenye mikutano ya mwaka ya Freemason Afrika
Mashariki ambayo imekuwa ikifanywa kila mwaka tangu mwaka 1989.
Hatua hiyo iliongezwa nguvu na baadhi ya viongozi
wasomi na wenye uelewa wa kutosha waliotoa mapendekezo mbalimbali ya
kuiimarisha Freemason. Hayo yote yalisaidia kuongezeka kwa mawazo mazuri
namna ya kuendesha Freemason.
Mwaka 1990 Afrika Mashariki ilishuhudia ujio wa wageni wakubwa
wawili; kiongozi mstaafu Lord Cornwallis na James Stubbs, waliowahi kuwa
viongozi wa juu wa Freemason.
Viongozi hao waliitembelea Tanzania na nchi
nyingine za Afrika Mashariki huku wakitoa mchango mkubwa uliosaidia
kuinua zaidi Freemason.
Wakiwa Dar es Salaam, Lord Cornwallis alikwenda
kuvua samaki katika Bahari ya Hindi na kurudi na aina ya samaki ambayo
haikuwahi kuonekana kwa zaidi ya miaka 50, jambo lililofanya samaki hao
kuitwa ‘samaki wa Cornwallis’.
Pia miaka ya 1990 ilitokea changamoto nyingine
iliyodumu kwa muda mfupi dhidi ya Freemason Afrika Mashariki, ikilenga
ofisi ya Kenya. Aliyekuwa Rais wa Kenya wakati huo, Daniel arap Moi
aliunda tume ya kuchunguza watu wanaoabudu shetani, ambapo moja ya
majukumu ya tume yalikuwa ni kuichunguza Freemason.
Nilifika mbele ya tume hiyo mara mbili katika
nyakati tofauti kama Mkuu wa Freemason Afrika Mashariki. Nilitoa
ushahidi kuhusiana na kazi tunazozifanya.
Nilipokwenda mara ya pili kukutana na tume hiyo,
tulitembelea ofisi ya Ukumbi wa Freemason wa Nairobi, huku tukiwa na
wapiga picha waliopiga picha nyingi sana.
Japokuwa tume haikutoa majibu ya kazi
waliyoifanya, tulipata taarifa kuwa walikuwa wametusafisha na tuhuma
zilizokuwa zinaikabili Freemason.
Nafurahi kusema kuwa tuhuma zile zilisafishwa
zaidi na Rais aliyefuata baadaye, Mwai Kibaki, ambaye katika moja ya
hotuba zake alisema kuwa Freemason imetoa mchango mkubwa sana Kenya.
Tangu wakati huo, aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa
Kenya wakati fulani, Moody Awori, alikuwa akiutembelea ukumbi wa
Freemason wa Nairobi na kunywa chai na baadhi ya wanachama. Pia alikuwa
akipokea michango mbalimbali iliyotolewa kwa vikundi na taasisi.
Toa Comment ili tuendelee
Toa Comment ili tuendelee