SOKA-BONGO: WAKATA MIWA KAGERA SUGAR WAPOKEA KIPIGO CHA 1-0 KUTOKA KWA MGAMBO.
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/09/soka-bongo-wakata-miwa-kagera-sugar.html
Klabu ya Mgambo JKT kutoka mkoani Tanga leo imewapigisha kwata wakata miwa wa Bukoba Kagera Sugar kwa kuichapa bao 1-0 katika mchezo wa ufunguzi wa ligi iliyochezwa katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Kagera sukari wamejikuta wakipokea kipigo hicho cha maumivi ya uchungu kutoka kwa maafande hao baada ya kushuka uwanjani kuzisaka pointi 3 za ligi kuu ya Vodacom lakini walishia kuziona zikipeperuka na kutua kwa wenyeji wao.
Mgambo katika msimu uliomalizika wa 2013/2014 iliponea chupu chupu kurudi ilikotoka kwa kushuka daraja na kuwaacha ndugu zao Rhino Rangers, Ashanti United pamoja na JKT Oljoro.