SIASA: VIONGOZI WA CHADEMA KUONJA CHUNGU YA KUFANYA MAANDAMANO BILA KIBALI
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/09/siasa-viongozi-wa-chadema-kuonja-chungu.html
Tundu Lissu akiwa na Viongozi wa Chadema mkoani Dodoma wanaoshitakiwa kwa kufanya kusanyiko bila kibali.
Viongozi wa Chadema wa mkoani Dodoma wako matatani baada ya
kushitakiwa kwa kosa la kufanya kusanyiko bila kibali mkoani humo mnamo
sept 18 mwaka huu.
Hatua hiyo imetokana na Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe kuitisha maandamano Tanzania nzima ya kupinga Bunge maalumu la katiba linaloendelea mkoani Dodoma hatua ambayo imepingwa vikali na jeshi la Poliisi nchini Tanzania.
Viongozi hao wote kwa pamoja wanatetewa na Mwanasheria wa chama hicho Tundu Lissu ambapo wameachiwa huru kwa dhamana.