SIASA: MNYIKA AANZA KUONESHA CHECHE ZAKE, AKOMALIA KUVUNJWA KWA BUNGE LA KATIBA
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/09/siasa-mnyika-aanza-kuonesha-cheche-zake.html
Hatimaye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), John Mnyika, bado ameendelea kulia na Bunge maalumu la katiba
ambapo amemtaka Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge hilo.
Aidha, Mnyika ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana wa vyama rafiki wa Chadema lengo likiwa ni kuwaandaa kwenye masuala ya uongozi.
Mafunzo hayo ni mwendelezo wa yale ambayo hutolewa na Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Afrika (DUA), kwa mwaka huu yamehusisha vijana kutoka Kenya, Uganda na Tanzania.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), Patrobass Katambi, amesisitiza kuwa wanataka katiba inayokubaliwa na Watanzania wote ambayo itakuwa na tija kwao.