jaridahuru

Mitandao

SIASA: URAIS 2015 WAZIDI KUONGEZA IDADI YA "WANAOUTAKA" , MAMA NYERERE NAE AMNADI MAKONGORO NYERERE



Dar es Salaam. Mke wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere amesema kuwa mtoto wake, Makongoro Nyerere ana haki ya kugombea nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Ijumaa wiki iliyopita, Makongoro alilieleza gazeti hili kuwa uamuzi wake kuhusu kuwania kiti hicho utajulikana mara kipenga kitakapopulizwa na CCM.
Kauli ya Makongoro ilitokana na uvumi uliokuwa umeenea katika mitandao ya kijamii kuwa mtoto huyo wa tano wa mwalimu Nyerere alikuwa anaandaliwa na watu waliofanya kazi karibu na mwalimu awanie nafasi hiyo.
Akizungumza na waandishi ya habari nyumbani kwake Msasani  jana, Mama Maria alisema mwanaye ana haki ya kugombea.
Mama Maria aliyekuwa ameawaalika waandishi wa habari kuzungumzia uvumi uliosambaa kuwa amefariki dunia, alitoa kauli hilo baada ya kuulizwa kama uvumi huo unahusiana na habari kuwa mwanaye anataka kugombea urais.
Alisema, “Hapana. Hayo mambo hayahusiani na mwanangu kutaka kuwania urais… yeye ni raia wa Tanzania na hiyo ni haki yake ya msingi,”
Pia, alidokeza kuwa wakati akizungumza na mwanaye mwingine juzi baada ya uvumi wa kifo chake, naye alimwambia kuwa anataka kuwania nafasi hiyo.
Akitoa ufafanuzi kuhusiana na uvumi huo alisema kuwa, taarifa za uvumi wa kifo chake zilikuwa za furaha kwake na wala siyo za huzuni kama watu wengi walivyodhania.
 “Tumekuwa tukifanya maombi ya kusali na kufunga kwa siku 40 kabla ya kipindi hiki cha Kwaresima kwa ajili ya kuliombea taifa na dunia kwa ujumla. Na sasa tunafunga tena, hivyo kwangu jambo hilo ni majibu ya maombi tunayofanya. Nimefurahia kwa sababu naona maombi yanafanya kazi. Haya ni majibu, tunasema tumepita mashetani,”alisema Mama Maria huku akitania kuwa karne hii ni ya kisasa kweli, hata marehemu anaongea.
Aliongeza;  “Baada ya kupokea taarifa hizo, kwa kuwa nilikuwa nimelala nilichofanya niliamka nikasali…nadhani Watanzania wanahitaji sana kusali, sala na kazi. Kama Taifa pia tunahitaji kuwa na siku moja maalumu ya maombi.”
Licha ya kusema kuwa taarifa hizo zilikuwa za furaha kwake, Mama Maria alisema taarifa hizo zilizua hofu kubwa kwa familia yake na Taifa zima kwa ujumla.
Alisema juzi mchana alianza kupokea simu kwa wingi tofauti na ilivyo kwa siku za kawaida.
Hata hivyo, alitoa angalizo kuwa huenda uvumi huo ukawa unahusiana na harakati za Uchaguzi Mkuu ujao.

Related

SIASA: CHADEMA YAIGEUKA UKAWA, YASEMA MBOWE ASIWAFANYIE MAAMUZI. YATOA TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA TAARIFA YA BAADHI YA WAJUMBE WA BARAZA KUU NA MKUTANO MKUU CHADEMA MIKOA YA DSM, PWANI NA TANGA KUPINGA UHUNI WA KISIASA UNAOITWA UKAWA. UTANGULIZI. Ndugu wanaHabari, T...

SIASA: "UKAWA NI KAMA BOKO HARAM" Nape Nnauye

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ni kundi  hatari linaloeneza chuki na kusambaza uongo...

SIASA: VIONGOZI WANAO WABEZA WABUNGE KUTAJWA BUNGENI

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amemtaka Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kusini Deosderius Mipata (CCM) kuwataja viongozi wa Serikali wanaobeza wabunge katika suala zima la utekelezaji wa maendeleo katika maene...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item