jaridahuru

Mitandao

GGM KUKABILIANA NA UHABA WA AJIRA!


KUTOKANA na uhaba wa ajira kwa vijana Mkoani Geita, Mgodi wa dhahabu wa Geita GGM umebuni miradi mbalimbali yenye lengo la kukabiliana na wimbi hilo ili kubadili na kukuza uchumi wao na jamii kwa ujumla ambapo zaidi ya vijana 400 wakiwemo wanawake watanufaika.

Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na ushonaji wa nguo, uchomeleaji , kilimo cha kisasa cha mpunga na uzarishaji wa tofari za kisasa, ambapo Mgodi huo kupitia kwa Makamu wa rais ambaye anashughulika na masuala ya jamii na maendeleo endelevu ilipo migodi ya Anglogold Ashanti duniani David Noko amesema mgodi utaendelea kuwahamasisha kuzalisha bidhaa iliyo bora itakayokidhi masoko yaliyopo nje ya Mkoa wa Geita.

Wakizungumza na CLOUDS baadhi ya vijana waliochukua fursa ya kujiunga na ujasiliamali katika moja ya mradi uliofadhiliwa na mgodi wa kuzalisha tofari za kisasa, pamoja na changamoto zilizopo kwa hivi sasa wamesema wamepokea mradi huo kwa matumaini ya kuwainua kiuchumi.

Awali akizungumza na baadhi ya vijana wakati alipotembelea kalakana la miradi hiyo, David Noko amesema kwamba miaka kadhaa iliyopita mgodi haukuwa na ukaribu na wananchi, lakini kwa hivi sasa anafarijika kuona mabadiliko ya kimahusiano yanaendelea kuonekana.

Pia Kiongozi huyo ametembelea maduka makubwa yanayoshirikiana na mgodi katika ununuzi wa bidhaa zake huku akidhuru kwenye mashimo yanayotoa dhahabu ndani ya mgodi wa GGM.

Related

Jamii 10755791366807548

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item