SIASA: WANACHAMA WA CHADEMA WAKAMATWA NA POLISI MOROGORO KWA KUFANYA MAANDAMANO BILA KIBALI

Wanachama waliokamatwa ni pamoja na Witnes Makoyola ambaye ni katibu wa Chadema tawi la kiwanja cha ndege, Shukuru Makamba, Maria Lissu, Hussein Hassan pamoja na Odwin Peter mkazi wa kiwanja cha ndege.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul wanachama hao walitenda tukio hilo katika maeneo ya mtaa wa Konga.
Ameongeza kwamba jeshi hilo liliwazuia wanachama kuandamana lakini hawakutii agizo hilo ambapo jeshi la Polisi liliwatawanya kwa mabomu ya machozi sambamba na kuwakamata watuhumiwa hao ambapo watafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.