SIASA: KIU YA URAIS 2015 YAMPONZA PINDA, JUKWAA LA KATIBA LADAI IMEZOROTESHA UTENDAJI SERIKALINI

Pinda aliyekuwapo jijini Mwanza kwa ajili ya kuendesha harambee ya Mfuko wa Taasisi ya Benjamin Mkapa iliyofanyika wiki iliyopita, alikutana kwa ‘mafungu’ na wajumbe zaidi ya 50 kutoka Mara, baadhi toka Mwanza, Geita na Kagera.
Aidha, Jukwaa la Katiba nchini limeibuka na kusema kuwa kitendo alichokifanya Waziri huyo mkuuu kimezorotesha utendaji serikalini, hii ni kutokana na kauli hiyo kuchochea uhasama kwa watumishi wa Umma.
Kwa mujibu wa Kaimu Mwenyekiti wa jukwaa la Katiba nchini Hebron Mwakagenda ambapo amesema Waziri mkuu huyo alikosea kuzungumza nia yake mapema huku akijua bado ni msimamizi wa Shughuli za serikali. Kaimu mwenyekiti amesema hayo katika mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dares salaam.
Amesisitiza kuwa Taifa litegemee kusinyaa kwa utendaji serikalini kutokana Nia hiyo aliyotangaza Waziri mkuu kwani sasa wakuu wa Wilaya na Mikoa wameanza kujigawa kimakundi na kila mtu kuanza kipigia debe upande wake anaoutaka na kuleta misuguano ndani ya Serikali.