CURLING: VAN GAAL WA MAN U ADAI ALITEGEMEA KIPIGO WALICHOPATA CHA 4:0 USIKU WA JUMANNE
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/08/curling-van-gaal-wa-man-u-adai.html
Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amesisitiza kuwa
“hakushtushwa kamwe” kwa kikosi chake kukubali kipigo cha mabao 4-0
kutoka kwa Milton Keynes (MK) Dons, katika mechi ya Kombe la Capital One
juzi usiku.
Man United ilitupwa nje ya michuano hiyo na kikosi cha Dons
kinachoshiriki League One, na kumuacha Van Gaal akiwaongoza Mashetani
Wekundu hao wa Old Trafford bila kuambulia ushindi katika mechi tatu
mfululizo za kimashindano tangu alipoanza kaazi.
“Mimi binafsi sikushtushwa na kipigo hiki, kwa sababu nilijua nini
kitatokea,” alisema Van Gaal na kuongeza: “Timu mpya kamwe haiwezi
kujengwa kwa mwezi mmoja.
“Lakini pia nadhani Milton Keynes walicheza vizuri sana, walikuwa
makini na mwisho wa yote walikuwa na bahati ya kupata mabao,” alisema
Van Gaal kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi aliyechukua mikoba
ya David Moyes.
Kosa lililofanywa na beki Jonny Evans lilimzawadia Will Grigg bao la
uongozi na mshambuliaji huyo wa MK Dons alifunga la pili baada ya saa
moja tangu bao hilo. Mshambuliaji wa Arsenal anayecheza Dons kwa mkopo,
Benik Afobe alifunga mabao mawili katika mechi ambayo Man United ilipiga
mashuti mawili tu langoni kwa wapinzani.
Van Gaal alienda mbali kwa kusema aliamua kupanga kikosi tofauti
katika jaribio la kukiangalia kikosi cha pili cha timu yake baada ya
sare ya mwishoni mwa wiki iliyopita ya bao 1-1 dhidi ya Sunderland na
kukiri namna kikosi chake kilivyokithirisha makosa.
“Tulifanya makosa mengi mno mchezoni. Mimi sijutii uteuzi wangu wa kikosi, lakini mabadiliko yalikuwa hatari kwetu.
“Nililazimika kubadili mfumo tuliochezea katika kipindi cha kwanza.
Tulicheza mmoja dhidi ya mmoja kwa kikosi kizima uwanjani na nadhani
uliliona hilo. Tulitengeneza nafasi nyingi, lakini kamwe hatukuwa na
bahati,” alisema Van Gaal.
Van Gaal alichukua mikoba ya kufanya kazi Old Trafford kiangazi hiki,
akibeba hatamu za Moyes, aliyeiongoza timu kumaliza Ligi Kuu ikiwa
nafasi ya saba, katika msimu ulioweka rekodi ya matokeo mabaya zadi kwao
kwenye historia ya Ligi Kuu.
Man United ikamtimua kazi Moyes mechi chache kabla ya kumaliza msimu,
na ujio wa Van Gaal ukaenda sambamba na matumizi makubwa ya fedha
katika usajili, ambako tayari imetumia kitita cha pauni mil. 131.7,
zikiwamo pauni mil. 59.7 ilizotumia Jumanne kumnasa winga Angel Di Maria
kutoka Real Madrid.