UEFA: SANCHEZ AIPAISHA ARSENAL KUINGIA HATUA YA MAKUNDI BAADA YA KUPACHIKA GOLI LA KWANZA ARSENAL.

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/08/uefa-sanchez-aipaisha-arsenal-kuingia.html
Mchezaji kutoka chile aliyekuwa akikipiga Barcelona na kununuliwa Arsenal Alexis Sanchez, ameipa timu ya Arsenali nafasi ya kuingia hatua ya makundi katika klabu bingwa ulaya baada ya kucheka na nyavu kwa mara ya kwanza toka atue klabuni hapo.
Sanchez ambaye alimalizia kazi nzuri ya jack wilshere alitupia goli hilo mnamo dakika ya kwanza ya nyongeza ya kipindi cha kwanza.
Hata hivyo kipindi cha pili kilionekana kuwa kigumu zaidi hasa baada ya beki wa arsenal Mathieu Dibuchy kupewa kadi ya nyekundu na kutoka nje.
Washika mitutu hao walijitahidi kuzuia goli hadi mpira unaisha ikawa ni Arsenal 1:0 Besiktas
FULL-TIME: Arsenal 1-0 Besiktas (agg 1-0)
Arsenal qualify for the Champions League group stage.