KITAIFA: TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAIOMBA SERIKALI KUCHUKUA HATUA KALI DHIDI YA WAUAJI WA ALBINO
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/08/kitaifa-tume-ya-haki-za-binadamu.html
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora(THBUB) imeiomba Serikali
kufanya jitihada kubaini wanaofadhili na kutekeleza vifo vya Albino.Kwa
mujibu wa Kamishna wa Tume hiyo Ali Hassan Rajabu vitendo hivyo vinaenda
kinyume na katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977
kifungu cha 12(2) kinachoitaka jamii kutambua na kutathmini utu wa mtu
na kifungu cha 14 kinachotaka kila mtu kupata hifadhi ya maisha yake.
Bw. Rajabu ametoa kauli hii leo mjini Dar es Salaam katika taarifa ya vyombo vya habari ambayo inalaani mauaji na ukataji wa viungo vya albino vilivyotokea hivi karibuni hapa nchini.