TZ: MOROCCO YAITOLEA NJE TAIFA STARS MECHI ILIYOOMBA YA KIRAFIKI, SASA TAIFA STARS YAWAMEZEA MATE WARUNDI
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/08/tz-morocco-yaitolea-nje-taifa-stars.html
Baada ya kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Mart Nooij kutangaza
kikosi kitakacho cheza na timu ya Taifa ya Morocco mchezo wa kirafiki
hapo Septemba 5, waarabu hao wamefuta ombi lao la kujipima na Tanzania
kama walivyo oba awali.
Morocco ndio iliomba kucheza na Tanzania katika tarehe hiyo lakini
wametuma ujumbe katika shirikisho la soka Tanzania kuwa hawata weza
kucheza mchezo huo.
Akizungumza na mwandishi wetu Katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa
amesema kuwa Morocco wameghairi kucheza wakidai kuwa asilimia kubwa ya
wachezaji wa timu hiyo wako kwenye michuano mbali mbali kwenye klabu zao
na hivyo hawata weza kuacha na kuja kucheza mchezo wa kirafiki.
Baada ya Wamorocco hao kujiondoa huku kikosi cha Taifa Stars
kikitarajia kuingia kambini Agosti 31, Kocha mkuu Nooij ameamua
kuichagua Burundi ili waweze kujipima katika tarehe hiyo.
Kwa mara ya mwisha Tanzania na Burundi zilipokutana Stars ililala
chini kwa kichapo cha bao 3-0 mbele ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dk. Jakaya M. Kikwete katika sherehe za muungano.