KIMATAIFA: ISRAELI YAANZA MASHAMBULIZI UPYA GAZA BAADA YA KUISHA MASAA SABA YA KUSITISHA MAPIGANO

Japokuwa kumekuwa na kupungua kwa kiwango cha mashambulizi nyakati za mchana, Wapalestina wameilaumu Israel kwa kuikuka walichokipanga wenyewe cha usitishaji wa mapingano na badala yake ikashambulia kwa bomu kambi ya wakimbizi katika eneo la kaskazini mwa Gaza na kuua mwanamke mmoja na mtoto wa miaka nane.
Israel imesema kwamba wapiganaji wa kiislamu wameendeleza upigaji wa mabumu katika ardhi ya Israel.
Katika mji wa Jerusalemu, Israel mwisreel mmoja aliuawa wakati trekta ya kuchimba mchanga ilipogonga basi jambo ambalo Israel imesma ni shambulio la kigaidi.