
Daktari aliyemtibu mgonjwa wa Ebola ameabukizwa nchini Nigeria
Daktari mmoja jijini Lagos
Nigeria aliyemtibu mgonjwa aliyefariki kutokana na homa ya Ebola
amepatikana ameambukizwa na maradhi hayo.
Daktari huyo ambaye alimtibu mfanyikazi wa
wizara ya hazina nchini Liberia aliyepatikana na homa hiyo ya Ebola na
kuwa mtu wa kwanza kuaga dunia nchini Nigeria sasa amedhibitishwa
kuambukizwa .
Waziri wa afya nchini humo Onyebuchi Chukwu
amesema kuwa daktari huyo pamoja na watu wengine 70 waliokutana na
marehemu wametengwa kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Mataifa yaliyoathirika na homa ya Ebola
Patrick Sawyer alitua nchini Nigeria Julai tarehe 20 na akafa tarehe 25 katika hospitali moja mjini Lagos.
Mlipuko huu wa ugonjwa wa ebola katika ukanda wa
magharibi mwa Afrika umesababisha vifo vya watu zaidi ya 826 katika
mataifa ya Guinea, Liberia na Sierra Leone.