EBOLA: KIGOMA YAANZA KUCHUKUA TAHADHARI ZA KUJIKINGA NA UGONJWA WA EBOLA KUFUATIA KUINGIA KWA EBOLA CONGO
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/08/ebola-kigoma-yaanza-kuchukua-tahadhari.html
Kufutia kuenea taarifa ya kuwepo wagonjwa nane wenye ugonjwa wa ebola
nchini Congo DRC, Mkoa wa kigoma umeamua kuchuakua hatua kukabiliana na
maingiliano ya watu mkoani humo.
Aidha, kutoakana na ujirani wa mkoa wa Kigoma na Congo DRC mkuu wa mkoa wa Kigoma Ndugu Issa Machibya amesema kwamba mkoa huo umeanza kuchukua tahadhari kwenye mipaka wa Tanzania na Congo DRC.
Ameongeza kwamba “ nimemuagiza katibu tawala wa mkoa magari yote yenye uwezo wa kubeba vipaza sauti usiku au jioni watu wamesharudi nyumbani yapite kutangazia Wananchi kwa muda wa siku tatu mfululizo licha ya kuweka vipeperushi kuhusu dalili na jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa ebola”
Kwa upande wa John Ndunguru katibu tawala wa mkoa amesema hospitali za mkoa huo zimeshatenga chumba maalumu ili kama mgonjwa akitokea awekewe kinga au wigo kwa muda wa siku 48.