UN: NCHI YA SYRIA YADAIWA KUKIUKA HAKI ZA BINADAMU, WATOTO WALAZIMISHWA KUJIUNGA NA ISLAMIC STATE
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/08/un-nchi-ya-syria-yadaiwa-kukiuka-haki.html
Umoja wa Mataifa umewashtumu , wanamgambo wa Islamic State kwa
kuwahujumu watu mara kwa mara mbali na kuwasajili watoto kujiunga na
jeshi wawe wanajeshi.
Wakati huohu UN imeistuhumu serikali ya Syria kwa kutumia kemikali aina ya Chlorine katika matukio manane katika ripoti mpya kuhusu uhalifu wa vita nchini humo.
Islamic State ambayo kwa sasa inadhibiti sehemu kubwa ya Syria ni moja ya vikundi ambavyo vinapigana na serikali ya rais wa Syria ,Bashar al-Asaad. Zaidi ya watu laki mbili wameuawa tangu vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe kutibuka mwaka wa 2011.
Ripoti hiyo inaeleza kwamba miili ya wale walio uawa huwa inawekwa kwa maonyesho kwa siku kadhaa kitu ambacho hutishia wakazi wa huko. Wanawake wamepigwa kwa kutovalia hijabu huku wale wanaoshtumiwa kwa usherati wakipigwa mawe hadi kufa hadharani.
Mjini wa Raqqa, watoto wadogo wenye umri wa miaka 10 wanapewa mafunzo katika kambi za IS suala ambalo ni kinyume kabisa na haki za watoto.
Kwa upande mwingine Paulo Pinheiro, alionya kuwa kundi hilo IS litaathiri eneo zima la ghuba.”Jamii ya kimataifa ilifeli kutekeleza wajibu wake mkubwa wa kulinda maisha ya raia dhidi ya ukiukwaji wa haki zao za kibinadamu.