jaridahuru

Mitandao

AFYA: EBOLA YAZIDI KUITESA LIBERIA, WAZIRI WA AFYA KIRI KUZIDIWA KUUDHIBITI ALAZIMIKA KUOMBA MSAADA

Waziri wa habari wa Liberia amekiri kuwa jinsi ugonjwa wa ebola unavotapakaa umezidi nguvu za huduma za afya za nchi.
Lewis Brown ameiambia BBC mfumo wa afya umefikia kikomo lakini alikanusha tuhuma kuwa serikali ilichelewa kuchukua hatua, akisema kuwa wakuu wanafanya wawezalo kukabiliana na janga wasilopata kukumbana nalo.
Alisema wananchi wengi bado hawakukubali ukweli halisi kuhusu ebola.
Shirika la msaada wa matibabu la kimataifa, MSF (Medicins Sans Frontiers), limesema kwamba makisio ya wizara ya afya ya Liberia ni madogo ikilinganishwa na ukweli ulioko nchini.
Hapo Jumamosi polisi wa kupambana na fujo walivunja maandamano dhidi ya serikali kwa namna ilivoshughulikia hali hiyo.
Inakisiwa kuwa ebola imeuwa watu karibu 1,000 nchini Liberia, Guinea, Sierra Leone na Nigeria.CRDT BBC SWAHILI

Related

Jamii 6241177260795790111

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item