jaridahuru

Mitandao

MICHEZO: TAIFA STARS KUIVAA MAMBAS YA MSUMBIJI UWANJA WA TAIFA JUMAPILI TAREHE 20/07/2014


KIKOSI cha timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), kimerejea jijini Dar es Salaam jana kutoka Mbeya ambapo Jumapili hii kitapambana na Msumbiji (Mambas) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kikosi hicho kinachoongozwa na Kocha Mkuu Mart Nooij, kilirejea jana asubuhi kwa ndege kutoka jijini Mbeya ambako kilipiga kambi ya wiki moja tangu kiliporudi nchini kutoka kambi nyingine ya mazoezi mjini Gaborone nchini Botswana.

Stars sasa imekamilika kwani Jumatano wiki hii, walitua wachezaji wawili nyota, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wakitokea Tunisia ambako klabu yao ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imeweka kambi ya mazoezi.

Naye mchezaji Mwinyi Kazimoto aliwasili jana 1.30 asubuhi kwa ndege ya Qatar Airways kutoka Qatar ambapo anacheza mpira wa miguu katika klabu ya Al Markhiya ya huko.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imepiga kambi katika Hoteli ya Protea Courtyard. Leo benchi la Ufundi la Taifa Stars pamoja na wachezaji watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli hiyo kuzungumzia maandalizi ya mechi yao.

Katika hatua nyingine, timu ya Taifa ya Msumbiji inawasili Dar es Salaam leo kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mambas itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7.30 mchana kwa ndege ya LAM ikiwa na msafara wa watu 37 ambapo kati ya hao, 25 ni wachezaji.

Wachezaji kwenye msafara huo ni Almiro Lobo, Apson Manjate, Bone Mario Uaferro, Dario Ivan Khan, Edson Sitoe, Eduardo Jumisse, Gelicio Aurelio Banze, Helder Pelembe, Josemar Machaisse, Elias Pelembe, Isac Carvalho na Jeffrey Constatino.

Wengine ni Manuel Fernandes, Manuel Uetimane, Mario Sinamunda, Momed Hagi, Reginaldo Fait, Reinoldo Mandava, Ricardo Campos, Saddan Guambe, Simao Mate Junior, Soares Victor Soares, Stelio Ernesto, Vando Justino na Zainadine Junior.

Timu hiyo itafikia kwenye Hoteli ya Accomondia, na itaondoka Jumapili baada ya kumalizika kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Mahmoud Ashour.

Kufika hatua hiyo ya raundi ya pili, Stars iliitoa Zimbabwe kwa jumla ya mabao 3-2, baada ya kushinda bao 1-0 jijini Dar es Salaam, kabla ya kulazimisha sare ya mabao 2-2 ugenini Harare.

Ili kuingia katika hatua ya mwisho ya makundi katika Kundi F lenye timu za Zambia, Cape Verde na Niger, Stars haina budi kuishinda Mambas katika mechi ya keshokutwa na ile ya marudiano wiki mbili zijazo.

Related

Michezo 7510858344971442826

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item