jaridahuru

Mitandao

JAMII: MADADA POA WACHEZEA KICHAPO TOKA KWA MAUSTADHI KWA KUJIUZA MWEZI MTUKUFU

 Maustadh wakimuadhibu mmoja wa machangudoa hao.
MAUSTADH jijini Dar es Salaam wamefikia uamuzi mzito wa kutembeza bakora kwenye vijiwe korofi vya warembo wanaojishughulisha na biashara haramu ya kuuza miili almaarufu kama machangudoa au machangu kwa kile kilichodaiwa kuwa wanasafisha jiji kutokana na kero za vishawishi vya kuharibiwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.  Kwa mujibu wa sosi aliyewasiliana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, maustadh hao walianza oparesheni yao waliyoibatiza jina la ‘Safisha Jiji’ maeneo ya Sinza kwenye mitaa ya Shule ya Msingi ya  Mapambano na jirani na msikiti uliopo maeneo ya Afrika Sana.

 Wakati maustadh hao wakiwafungia kazi na kutembeza bakora, OFM ilifika maeneo hayo na kufanikiwa kunasa tukio zima ambapo iliwashuhudia warembo hao waliokuwa wakijiuza kwa madai ya kusaka fedha za sikukuu, wakipewa kibano cha kutosha.
Mmoja wa machangudoa hao akidhibitiwa.
 Wakizungumza na OFM baada ya sakata hilo, maustadh hao walisema wamechoshwa na uchafu unaofanyika kwenye makazi yao huku wakifunguka kuwa mara kadhaa wanaporudi nyumbani wakitokea msikitini, machangu hao huwang’ang’ania wakiwashawishi kufanya nao ngono bila kujua wapo katika mfungo.“Tumechoshwa na ufuska, mbaya zaidi hawa machangu wanafikia hatua ya kutung’ang’ania wakitulazimisha tuwanunue bila kujali kama tunatoka msikitini kuswali,” alisema mmoja wa maustadh hao na kuongeza kuwa wanauheshimu mwezi huu mtukufu ndiyo maana wameamua kutembeza bakora kwa machangu hao.
 Warembo hao walishuhudiwa wakiwaomba msamaha maustadh hao na kudai kuwa wamekoma, hawatarudia tena kuwasumbua maustadh.“Jamani kaka zangu nawaomba msinichape sana nina ujauzito, naomba mnichape kwenye makalio nimekoma sitarudia tena,” alisema mmoja wa machangudoa aliyekuwa akitembezewa kichapo. Imeandaliwa na Shani Ramadhani, Deogratius Mongela na Chande Abdallah

Related

Jamii 1812075975459024814

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item