jaridahuru

Mitandao

KITAIFA: ABIRIA WA BODABODA SASA KUKAMATWA, NI WATAKAOPANDA PIKIPIKI MAENEO YA KATIKATI YA MJI DAR


MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Massaburi amesema abiria watakaokutwa wakiwa wamepanda pikipiki (bodaboda) katika maeneo ambayo pikipiki hizo hazina leseni ya kufanya biashara, watakamatwa na kufikishwa mahakamani pamoja na dereva.

Alisema pia wafanyabiashara ndogo, watakaokutwa wakifanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria, ikiwemo maeneo ambayo yamefanyiwa usafi na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam hivi karibuni, watakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Alisema hayo mjini Tanga jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambao walitaka kufahamu msimamo wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), kuhusu waendesha bodaboda katika maeneo mbalimbali nchini.

Dk Massaburi mbaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa ALAT, alisema Jumuiya hiyo imekuwa bega kwa bega na kuwaunga mkono waendesha bodaboda nchini, pale wanapofanya biashara zao kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.

Akizungumzia agizo la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam la kuwazuia waendesha bodaboda na wafanyabiashara ndogo, kufanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria, ikiwemo kuingia katikati ya Jiji, Dk Massaburi alisisitiza kuwa agizo hilo liko pale pale, kwa vile lipo kisheria.

Alisema ili kuonesha kuwa Halmashauri ya Jiji inatilia mkazo agizo hilo, kuanzia sasa abiria atakayekutwa akiwa amepanda pikipiki katika eneo ambalo haina leseni ya kufanya biashara hiyo, atakamatwa sambamba na dereva na kufikishwa mahakamani mara moja.

Alisema hatua kama hizo pia zitachukuliwa kwa wafanyabiashara watakaokutwa wakifanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria yakiwemo yale yaliyovunjwa na Jiji hivi karibuni katika operesheni ya kusafisha Jiji la Dar es Salaam.

Related

Kitaifa 4869940243211626392

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item