KIMATAIFA: SASA NJAA NA MAGONJWA YAIKUMBA SUDAN YA KUSINI BAADA YA MAKUBALIANO YA KUSITISHA VITA

Umoja wa Mataifa umeomba mchango wa dola bilioni moja kuwasaidia watu walioathirika na vita Sudan Kusini.
Baada ya miezi sita ya mapigano mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa, Toby Lanzer, amesema watu milioni 7 wako katika hatari ya njaa na magonjwa.
Alieleza kuwa wengi waliokimbia makwao wanaishi kwenye matope kwa sababu msimu wa mvua umeshaanza; malaria imezagaa na kipindupindu kimezuka.
Awali juma hili serikali ya Sudan Kusini na wapiganaji walikubaliana kusitisha vita, lakini siku za nyuma makubaliano kama hayo yalikiukwa haraka.