SIASA: LOWASSA AMPA SHAVU FILIKUNJOMBE, ASEMA NI KIONGOZI MWENYE MFANO WA KUIGWA

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/siasa-lowassa-ampa-shavu-filikunjombe.html
WAZIRI
mkuu wa zamani Edward Lowassa na wabunge mbalimbali wamempongeza
mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa jitihada mbali mbali za
kuwakomboa wana Ludewa.
Lowassa ambae ni mbunge wa jimbo la Monduli alitoa pongezi hizo mjini Dodoma juzi nje ya ukumbi wa bunge wakati akisalimiana na viongozi wa CCm ngazi ya kata zaidi ya 92 waliofika bungeni kushuhudia shughuli za bunge kwa mwaliko wa mbunge Filikunjombe.
"Wana Ludewa mna kila sababu ya kujivunia kwa kuwa na mbunge mchapa kazi ninyi mnamwita Jembe ila mimi namwona zaidi ya jembe ni katapila na hamkokosea kumchagua nawaombeni mtunzeni mbunge wenu na epukeni na michepuko kwani ni mbunge makini na anayependa kuwatumikia"alisema Lowassa
Mbunge wa jimbo la mbinga Magharibi kepten John Komba amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kutokana na jitihada mbali mbali anazoendelea kuzifanya katika kuwatumikia wana Ludewa.

Komba
ametoa pongezi hizo juzi wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha
wajumbe 92 kutoka jimbo la Ludewa ambao ni wenyeviti kata na
makatibu kata kutoka kata zote 25 za jimbo la Ludewa na viongozi
wa wilaya ambao wapo katika ziara ya siku nne mjini Dodoma na Dar
es Salaam .
Alisema
kuwa jembo kama Filikunjombe katika historia ya jimbo la Ludewa ni
aliyepata kuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Holace Kolimba na baada
ya hapo mbunge mchapakazi ni Filikunjombe .
“Nasema
mmlea Deo Filikunjombe ni mbunge atakayefanya makubwa jimbo la
Ludewa kutokanana jitihada zako za kimaendeleo na kazi kubwa
anayoifanya ya kuwatumikia wananchi wa jimbo la Ludewa ….nataka
kuwaambieni leo viongozi ambao mpo hapa Filikunjombe kwangu mimi
amekuwa msaada mkubwa sana”
Hata
hivyo alisema kuwa jitihada kubwa zimekuwa zikifanywa na Filikunjombe
pamoja na wabunge wengine wa mkoa wa Ruvuma ambao wanazunguka
ziwa nyasa kutokana na adha kubwa ya usafiri ila kwa sasa kero ya
usafiri ikiwemo ile ya mlima kandamija.
Pia
amewaonya wana Ludewa kuacha kutafuta mbunge kama ndugu yao na
badala yake kumtafuta mbunge wa ajili ya kuwapelekea maendeleo kama
ilivyo kwa mbunge huyo ambaye amekuwa ni mwabikaji mzuri kwa
wananchi.
“Mkimuacha
Deo Filikunjombe Ludewa mmekosa mambo na mmekosa maendeleo katika
jimbo hilo hivyo ni lazima kuendelea kumtunza ili azidi
kuwatumikia zaidi.”
Komba
alisema kuwa wilaya ya Ludewa mbali ya kuwa na utajiri mkubwa madini
ila wabunge wote waliopita walikuwa wakizungumzia suala hilo
bila kuonyesha jitihada ila toka ameingia Filikunjombe madini hayo
yameanza kushughulikiwa .
Alisema
kuwa kwa sasa wananchi wa Mwambao kilio chao kikubwa ni meli na
kuwa tayari wabunge wote wa Mwambao wameungana kuona wanapigania
upatikanaji wa meli hiyo ili kutatua kero ya usafiri ziwa Nyasa .
“Mwisho
nasema endeleeni kumpatia ubunge Deo Filikunjombe msibadilishe wabunge
kama gauni…wenzetu wa kaskazini wanatushinda katika hilo mfano Msuya
aliacha ubunge baada ya kusema mwenyewe sasa basi baada ya
kufikisha maendeleo makubwa ikiwa ni pamoja na kufikisha umeme hadi
chooni ….ila sisi baada ya kipindi kimoja tunasema aliyevivyo(amekula
hivyo hivyo)”alionya Komba .
Huku kwa
upande wake , Mbunge wa Mbinga Mashariki Gaudence Cassian Kayombo
alisema kuwa mbali ya wana Ludewa kumuona mbunge wao ni jembe ila
kwake na wabunge wengine na kusini wamekuwa wakimuona ni mkombozi
wa maendeleo mikoa ya kusini.
Kayombo
pia amewaonya wana Ludewa kuachana na tabia ya kubadili wabunge
kama nguo na kuwa iwapo mbunge wao asingekuwa mchapakazi ni wazi
harufu ya upinzani ingeanza kujitokeza katika jimbo hilo ambalo
limeendelea kuwa ni tishio hata kwa vyama vya upinzani .
Kwani
alisema jitihada za wana Ludewa kujaribu kwa sasa zimefika kikomo
baada ya kumpata mbunge huyo ambae ni mchapakazi mzuri na kuwa ni
vema wana Ludewa hawana haja ya kuendekeza uchoyo .
“Kitu
ambacho kitaendelea kuiweka CCM madarakani ni umoja na mshikamano na
bila umoja na mshikamano hakuna chama na hakuna mbunge ndani ya CCM”
Kwa
upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Hilda Ngowi mbali
ya kumpongeza mbunge Filikunjombe kwa maendeleo bado alisema kuwa
mbunge huyo ameleta ngunzo kubwa bungeni kwa kuvunja rekodi ya
kukaribisha wageni wengi zaidi bungeni tukio ambalo ni la kwanza kwa
mbunge kuleta wabunge wengi kiasi hicho bungeni.
Huku
mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) akisema kuwa
anatamani sana kufika Ludewa ili kumuunga mkono mbunge Filikunjombe
ambae amekuwa ni ngunzo katika bunge kwa utendaji kazi na kutetea
maslahi ya wananchi wake na Taifa.
Mbunge wa jimbo la Mwibara Kangi Lugola alisema kuwa kamwe katika ubunge wake hatakuja kumsahau mbunge Filikunjombe na kudai kuwa lazima viongozi wa kata na wanachi wa jimbo la Ludewa kuachana na michepuko kwa kutazama huku na kule badala yake kutulia njia kuu kwa maana ya kuendelea kufanya kazi na Filikunjombe.

Wakati
Filikunjombe akidai kuwa wito ambao wajumbe hao wameonyesha ni wito
mzuri zaidi na kuwa hilo ni deni kwake na malipo yake ni
kuwafikishia maendeleo jimboni.
Kwani
alisema kuwa kamwe hatawaangusha katika utendaji kazi wake na kuwa
ni lazima aendelee kufanya kazi kwa moyo zaidi ili kuwapa imani
wananchi