jaridahuru

Mitandao

JAMII: SERIKALI YAONYA WANAOAJIRI WATOTO MIGODINI, YAHIMIZA SEKTA YA MADINI KUAJIRI WATAALAMU WAZAWA

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia madini Stephen Masele amekemea vikali tabia ya wamiliki wa migodi kuajiri watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 kwani inarudisha maendeleo ya watoto hao na kwa jamii kwa ujumla inayowategemea.

Waziri Masele ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa semina iliyoshirikisha wachimbaji wadogo, madiwani, viongozi wa vijiji, wilaya, madiwani pamoja na viongozi wa vyama vya siasa inayoendelea katika jimbo la Mwibara wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Waziri Masele alisema kuwa kumekuwepo na tabia ya wamiliki wa migodi, ikiwa ni pamoja na wazazi wenye watoto wenye umri chini ya miaka 18 kuruhusu watoto hao kufanya kazi kwenye migodi badala ya kuwahimiza kwenda shule na kupata elimu itakayowasaidia kutoka kwenye giza.
Kutokuwapeleka watoto shule na kuwahimiza kushiriki katika shughuli za madini ni  kuwaharibu kisaikolojia kwa kuwakosesha elimu kama haki  yao kimsingi, ni kosa kubwa sana. Alisema Waziri Masele.
Waziri Masele alieleza kuwa umefika wakati wa wamiliki wa migodi  pamoja na wazazi kuwahimiza watoto kuhudhuria shule ili kuweza kuwa wataalamu wa  kutegemewa baadaye katika taifa kama marubani, wahandisi,  mawaziri na madaktari.
Aliongeza kuwa mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kuwa kila sekta inasimamiwa na wataalamu ambao ni wazawa kwa kuhakikisha inalipa suala la elimu kipaumbele kikubwa.
Inatakiwa pindi migodi mikubwa itakapoanzishwa wataalamu wengi kwenye migodi wawe ni wazawa badala ya kuishia kuwa vibarua na nafasi zao kuchukuliwa na wataalamu kutoka nje.” Alisisitiza Waziri Masele.
Waziri Masele aliongeza kuwa  ili nchi  yeyote iweze kupiga hatua kimaendeleo inahitaji wataalamu katika kada mbalimbali na kuongeza kuwa serikali ipo  tayari kutoa msaada katika kuzalisha wataalamu hususani katika sekta za nishati na madini.
Akielezea mikakati ya  serikali katika kuimarisha sekta ya madini Waziri Masele alieleza kuwa serikali kupitia Wizara imeanza kufufua vyama vya uchimbaji madini  ikiwa ni pamoja na kuanza kutoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo kwani wana mchango mkubwa sana katika pato la taifa.

Waziri Masele alieleza kuwa serikali ilianza kutoa ruzuku na itaendelea kutoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo  watakaothibitishwa  na chama cha wachimbaji  madini kuwa wanajishughulisha na shughuli za uchimbaji madini  lengo likiwa ni kuboresha maisha yao.
Alitaja mikakati mingine kuwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu ya kanuni za uchimbaji bora na salama wa madini kwa kutumia wataalamu wake sehemu zote zenye madini nchini.
Akielezea  kanuni za uchimbaji salama wa madini Waziri Masele aliwataka wachimbaji wadogo kuachana na matumizi  ya zebaki katika uchenjuaji madini kwani zina athari kubwa kiafya na badala yake watumie cyanide.
Waziri Masele alisema kuwa matumizi ya zebaki yana athari kubwa kwa mchimbaji madini ikiwa ni pamoja na jamii inayomzunguka na hata vizazi vijavyo.
Alitaja athari za zebaki ni pamoja na magonjwa ya  kansa, pamoja na kuwa na kuwa na vizazi vya watoto wenye ulemavu wa mtindio wa  ubongo.
Unajua athari hizi zinaweza kuonekana hata baaada ya muda mrefu, watu wanaweza kuathirika kwa kula viumbe  kama samaki vilivyoathiriwa na zebaki iliyotokana na maji yaliyooshea madini hayo kutiririshwa ziwani au kwenye mito.” Alisisitiza
Waziri Masele aliwataka wachimbaji wadogo kufuata kanuni za umiliki leseni  ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza kati yao na wamiliki wa migodi.
Waziri Masele aliongeza kuwa kumiliki ardhi hakutoshi kumpa uhalali mmiliki wa eneo husika kuchimba madini kwani ardhi ni eneo la juu likiwa ni pamoja na mimea na mito na si madini yaliyopo chini yake.
Aliwataka wamiliki wa ardhi yenye madini kuomba leseni ya uchimbaji madini ili kuweza kuchimba madini au kuingia ubia na wenye kuhitaji maeneo yao.



Related

Jamii 3989057552650952548

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item