jaridahuru

Mitandao

JAMII: BAADA YA SKENDO YA MHE. KOMBA, MAKAHABA WASAKWA DODOMA, WANASWA 4 WA KINYARWANDA

 
Wanawake wanne raia wa Rwanda wametiwa mbaroni mjini Dodoma kutokana na kuingia nchini kinyemela na kujihusisha na biashara ya ukahaba.
 
Watuhumiwa  watatu kati ya hao, Saidat  Umotoni (28), Asha Abimana (25) na Asia Umotoni  Wase (30), hii ni mara yao ya pili kukamatwa mjini hapa wakidaiwa kujihusisha na biashara hiyo.
 
Mara ya kwanza ilikuwa Novemba mwaka jana ambapo wote  ( Asia, Asha na Saidat) baada ya kukamatwa, walirudishwa kwao baada ya kulipa faini.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma,  Proches Kuoko, alimtaja mwingine aliyekamatwa ni Chalote Uwase (28) ambaye ameshahukumiwa kifungo cha miaka miwili anachotumikia katika Gereza la Isanga, mjini hapa.
 
Alisema wahamiaji hao wote kwa pamoja walikamatwa na maofisa wa kikosi cha Uhamiaji, baada ya kupata taarifa kwa kuwepo raia hao katika eneo la barabara ya Bahi ndani ya Manispaa ya Dodoma.
 
Alisema wanawake hao walikamatwa  usiku kwenye mitaa hiyo huku wakiwa kwenye harakati za kutafuta  wateja na walipohojiwa wote kwa pamoja hawakuwa na hati ya kusafiria na kuishi hapa nchini na walizokuwanazo zilikuwa zimeisha muda wake wa matumizi.
 
“Hata  walipopekuliwa,  walikutwa wakiwa na hati ya kusafiria iliyokuwa imeisha muda wake wa kuwawezesha kuishi hapa nchini na walipohojiwa zaidi walisema wao kazi yao ni uchangudoa,”alisema Kuoko.
 

Related

Jamii 2686433119379038766

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item