jaridahuru

Mitandao

KIMATAIFA: WATU 10 WAPOTEZA MAISHA NA ZAIDI YA 80 KUJERUHIWA KATIKA MILIPUKO YA MABOMU NAIROBI


Matukio ya Kigaidi yameendelea kuigubika nchi ya Kenya ikiwa ni pamoja na milipuko ya mabomu katika sehemu mbali mbali za nchi hiyo.

Leo katika hali isiyo ya kawaida milipuko miwili imeripotiwa katika sehemu mbili za maeneo ya soko la Gikomba lililoko katika mtaa wa Eastleigh Huko Mjini Nairobi. Watu 10 wamepoteza maisha na wengine 80 kulazwa katika hospitali mbali mbali za jiji hilo.


Kamanda wa polisi wa eneo hilo amethibitisha kutokea kwa milipuko hiyo na kuwaomba watu kuwa watulivu na kumripoti mtu yeyote wanaemhisi. Hata hivyo hakuna aliyekamatwa kwa kuhusika na tukio hilo ingawa taarifa za awali zinakihusisha kikundi cha Al-Shabab na tukio hilo.

Mlipuko wa kwanza ulitokea katika gari la abiria wakati la pili likitokea upande wa pili wa soko.
Milipuko ya leo imetokea siku moja baada ya Uingereza kutoa onyo kwa raia wake wanaoishi nchini humo kurejea makwao kwa hofu ya usalama na pia baada ya tahadhari kutolewa ya kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi nchini humo.

Gikombaa ni soko kubwa la kuuza nguo ambalo linapakana na mtaa wa Eastleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.

Soko hilo linapakana na mtaa wa Easleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.

Shirika la serikali la kushughulikia majanga linasema kuwa angalau watu 10 wamefariki na wengine zaidi ya 80 kujeruhiwa.


Related

Kimataifa 3624488940881322259

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item